Daktari feki akamatwa Mwanza

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714

Uongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure umemnasa mkazi wa Nyakato Mecco jijini Mwanza David Igwesa kwa tuhuma za kujifanya daktari na kupokea pesa toka kwa baadhi ya wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa upasuaji.

Daktari huyo ‘feki’ amekamatwa na uongozi wa hospitali ya Sekou Toure, baada ya kuomba shilingi laki tano kutoka kwa Bw. Tungu Sibula kwa ajili ya kumfanyia upasuaji baba yake mzazi, aitwaye Dotto Sibula mkazi wa Tinde Shinyanga, hata hivyo mgonjwa huyo alifanikiwa kulipa shilingi laki moja na elfu sabini tu, kati ya kiasi cha pesa alichoombwa na daktari huyo.
 
Maisha yamevaa pensi. Kila mtu anabuni mbinu mbadala za kupiga hela.

Watu wanafanya magumashi mpaka kwenye afya za watu directly!!! Si ajabu mtu kama huyo atahonga, figisu zitafanyika, kisha police wanafunika file anarudi uraiani.
 
Hapa sio pensi bali pampers kabisa
 
Hapa sio pensi bali pampers kabisa

hahahaa mkuu, ni sheedah aiseee.

Afu mkuu naomba unifundishe uchawi wa kupata hela. lol. maana maisha yanazidi kuvaa pampers kila kukicha

Bora tutumie ndumba kupiga hela, sio kucheza na afya za watu kama huyo daktari kanyaboya. Lol
 
Uko tayari kufanya kafara la damu?
 
jamaa alijieleza fresh tu kuwa anandoto za kuwa daktari hana hata woga ... jamani imekula kwake japo sijui wagonjwa wangapi kawatibu uongo
 
hahahaa mkuu, ni sheedah aiseee.

Afu mkuu naomba unifundishe uchawi wa kupata hela. lol. maana maisha yanazidi kuvaa pampers kila kukicha

Bora tutumie ndumba kupiga hela, sio kucheza na afya za watu kama huyo daktari kanyaboya. Lol
Mkuu ni afadhali ya huyo anayetapeli kuliko washirikina na wachawi wanaouwa vikongwe na albino
 
kwahiyo ni kishoka huyu akishapata pesa anatafuta daktari wanagawana puuumbacvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvvv
 
Wampe adhabu kali maana kuchezea maisha ya mtu kwa staili hiyo ni balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…