PROF NDUMILAKUWILI
JF-Expert Member
- Mar 25, 2016
- 10,518
- 13,135
heee hii sasa sio afya hapa kipindupindu kinamkamata by the way huduma ya kwanza ya kipindupindu ni ipi hahahah
Dah!!!umenikumbusha mbaaali.,tukiwa primary tukitoka shule jioni au hata after lunch (kama vipindi vya jioni sio tunatoroka)tulikuwa tuna~cross mto mmoja mpaana na wenye kina kwa kuogolea kwenda kuiba miwa mitam na laini(bungara asilia) kwenye shamba la mkulima wa kihindi."maisha ya utoto ni hatari sana sometimes kwani huko nyoka si wakuuliza na shughuli ipo wakati wa kurudi na shehana uliyovunja kwa tamaa.,yaani ubebe kidogo uogelee nayo ku~cross ama ubebe mingi uzungukie njia ndefu yenye nyoka zaidi ila upate ahueni ya kupita juu ya tindiga lililofunga majani ya kutambaa huku chini yake kina kirefu kama kawa.
Dah!!!ama kweli dunia tunapita kwani wenzangu wengi kati ya hao toto tundus washatangulia mbele ya haki.
"Eee MOLA WAREHEM".
Mwanzo umenifurahisha sana ila mwisho umenitia huzuni.Dah!!!umenikumbusha mbaaali.,tukiwa primary tukitoka shule jioni au hata after lunch (kama vipindi vya jioni sio tunatoroka)tulikuwa tuna~cross mto mmoja mpaana na wenye kina kwa kuogolea kwenda kuiba miwa mitam na laini(bungara asilia) kwenye shamba la mkulima wa kihindi."maisha ya utoto ni hatari sana sometimes kwani huko nyoka si wakuuliza na shughuli ipo wakati wa kurudi na shehana uliyovunja kwa tamaa.,yaani ubebe kidogo uogelee nayo ku~cross ama ubebe mingi uzungukie njia ndefu yenye nyoka zaidi ila upate ahueni ya kupita juu ya tindiga lililofunga majani ya kutambaa huku chini yake kina kirefu kama kawa.
Dah!!!ama kweli dunia tunapita kwani wenzangu wengi kati ya hao toto tundus washatangulia mbele ya haki.
"Eee MOLA WAREHEM".
Aaamin.Beautiful story
Amina mungu awarehem
Aaamin.,pole kukuhuzunisha.,mie mwenyewe nilipoanza kuandika nilikuwa na kumbukumbu ya furaha nilivyokuwa ninaendelea kuandika ndipo nikaanza kuwakumbuka mmoja baada ya mwingine kwa tuliyokumbana nayo siku baada ya siku tukienda ama tukirejea na ndipo huzuni iliponiingia baada ya kumkumbuka best yangu na jirani yetu Ramadhan (R.I.P)ambaye nilikuwa ninaficha miwa yangu kwao kwani kuingia nayo home ilikuwa issue,ni bora nionekana nimepauka kwa kuogelea maji ya mtoni kuliko ijulikane nimeenda kuiba miwa kwenye shamba la nyoka.Mwanzo umenifurahisha sana ila mwisho umenitia huzuni.
Amen
Dah pole sana mkuu.Aaamin.,pole kukuhuzunisha.,mie mwenyewe nilipoanza kuandika nilikuwa na kumbukumbu ya furaha nilivyokuwa ninaendelea kuandika ndipo nikaanza kuwakumbuka mmoja baada ya mwingine kwa tuliyokumbana nayo siku baada ya siku tukienda ama tukirejea na ndipo huzuni iliponiingia baada ya kumkumbuka best yangu na jirani yetu Ramadhan (R.I.P)ambaye nilikuwa ninaficha miwa yangu kwao kwani kuingia nayo home ilikuwa issue,ni bora nionekana nimepauka kwa kuogelea maji ya mtoni kuliko ijulikane nimeenda kuiba miwa kwenye shamba la nyoka.
Akhsante mpendwa Nifah.,unajua yule mhindi alikuwa muungwana kiasi,aliruhusu watu kula palepale au kubeba mua usiozidi mmoja kwa mtu mmoja.,hivyo hata ilipotokea mkipiga kelele walinzi wake wakija wanatoa msaada na walikua wazoefu na mabingwa wa kutoa huduma kwanza kwa kufunga kuzuia sumu kusambaa then kuchanja ulipoumwa kukamua sumu na kupaka dawa za kiasili (mawe,majani) kufuatana na aina ya nyoka aliyekudhuru(ambazo walikuwa hawazikosi mifukoni mwao au katika migorori(mashuka)yao.Ninamshukuru Mungu katika team yetu hakuna aliyekutana na kadhia hiyo kwani tulishajua kujihami kwa kuchapa majani na fimbo ili nyoka wakimbie ila pia ilishawahi tokea sisi pia kukimbizwa na green cobra aliyekuwa anachunga mayai yake hadi kwenye maji mtoni then akarudi kwenda kuendeleza ulinzi wa mayai yake.,amini usiamini siku hiyo ham ilituisha na tulirudi kapa na kuacha hiyo tabia kwa wiki kadhaa.,pamoja na kua vituko haviishi mara huyu ataguswa na jani aamshe wenge wote mtoke nduki mara mwingine atishie tu ilmradi vituko kedekede.,yuko huyo bwana Petro alikuwa ni shida kwa vioja (ana vituko huyoo)na amekuja zamia zaidi kuwajua viumbe hawa na imekuja kuwa ndiyo kazi yake kuu ya kumwingizia kipato.Dah pole sana mkuu.
Sasa mimi nina swali,hamkuwahi kujeruhiwa hata mara moja ktk wizi wenu huo wa miwa?
Binafsi naogopa nyoka sana,napenda miwa ila siwezi kuhimili hofu ya kuumwa na nyoka.
Hahahaaaaaaaaa asante sana kwa story hii mkuu,umenifurahisha sana hasa mwishoni.Akhsante mpendwa Nifah.,unajua yule mhindi alikuwa muungwana kiasi,aliruhusu watu kula palepale au kubeba mua usiozidi mmoja kwa mtu mmoja.,hivyo hata ilipotokea mkipiga kelele walinzi wake wakija wanatoa msaada na walikua wazoefu na mabingwa wa kutoa huduma kwanza kwa kufunga kuzuia sumu kusambaa then kuchanja ulipoumwa kukamua sumu na kupaka dawa za kiasili (mawe,majani) kufuatana na aina ya nyoka aliyekudhuru(ambazo walikuwa hawazikosi mifukoni mwao au katika migorori(mashuka)yao.Ninamshukuru Mungu katika team yetu hakuna aliyekutana na kadhia hiyo kwani tulishajua kujihami kwa kuchapa majani na fimbo ili nyoka wakimbie ila pia ilishawahi tokea sisi pia kukimbizwa na green cobra aliyekuwa anachunga mayai yake hadi kwenye maji mtoni then akarudi kwenda kuendeleza ulinzi wa mayai yake.,amini usiamini siku hiyo ham ilituisha na tulirudi kapa na kuacha hiyo tabia kwa wiki kadhaa.,pamoja na kua vituko haviishi mara huyu ataguswa na jani aamshe wenge wote mtoke nduki mara mwingine atishie tu ilmradi vituko kedekede.,yuko huyo bwana Petro alikuwa ni shida kwa vioja (ana vituko huyoo)na amekuja zamia zaidi kuwajua viumbe hawa na imekuja kuwa ndiyo kazi yake kuu ya kumwingizia kipato.
Ahahaaaaaa sisi tulikuwa tunakwenda kuiba na kamba tunaifunga miwa na kamba kisha tunaifunga miguuni kisha tunaivuta mtu akiwa kwa mbali anaweza akashangaa mbona ni kiangazi lakini jamaa anatembea kama mtu anayetembea kwenye uterezi au anapanda mlima kilimanjaro kumbe huku chini tumesheheni mizigo kama trekta za kagera sugar.Nakumbuka siku moja mwenye shamba alitulia ambush akadaka mmoja akaja nae shuleni amembebesha begani miwa alokuwa amekwishaikata.Kengere ikagongwa akaletwa mbele na miwa yake AAHAHAAAAAAAAAA yaani huwa nikiikumbuka hiyo siku nacheka kabisa.Akaambiwa anza kuwaita wenzako tulipokea kichapo kutoka kwa waalimu wote walijipanga mstari unapita unapokea za kutosha unahamia kwa mwingine hadi waalimu wote.Sasa wanafunzi wasivyo na siri wakati tunaadhibiwa si wakatoa siri kwamba tena kwa sauti HUWA WANAKUJA NA MIWA KUTUUZIA HAPA SHULENI.
Hiyo ilikuwa primary mwaka 1995 nikiwa darasa la tano