Dada wa Barack Obama ashiriki katika Maandamano, arushiwa mabomu ya machozi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,510
6,005
Auma Obama, dada wa kambo wa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, amerushiwa mabomu ya machozi na Polisi wakati wa mahojiano na Kituo cha CNN alipokuwa akihojiwa wakati akishiriki katika Maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha.

Akizungumzia Maandamano hayo ya kupinga Muswada wa Fedha 2024, Auma huku amesema “Vijana wa Kenya wanaandamana wakiwa na bendera za Nchi yao kufikisha ujumbe wao lakini wanapigwa, kwanini unawapiga mabomu ya machozi vijana badala ya kuwasikiliza.”

Polisi jijini Nairobi wametumia mabomu ya machozi ya machozi kuwatawanya waandamanaji nchini humo wakati wabunge wa Kenya walipokuwa wakijadili muswada wa fedha unaopendekeza ongezeko la kodi kwenye mkate, umiliki wa magari, na miamala ya fedha.

================For English Audience Only======================

Auma Obama, the half-sister of former United States President Barack Obama, has been teargassed by police during an interview with CNN live on air, while protesting Kenya's controversial finance bill.​

Kenya is in the grip of nationwide protests against proposed tax hikes, culminating in a planned "total shutdown" of the country.

The demonstrations, sparked by the Finance Bill 2024, have seen citizens rally under the banner of "7 Days of Rage," as the nation faces more days of upheaval.

Source: CNN
 
Back
Top Bottom