Dada uliyesababisha ajali maeneo ya Bahari Beach ukipona nitafute

canular

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
889
866
Wakuu heshima yenu nawapa, madogo marahabaa

Aisee wakuu Jumapili ya leo katika mazingira fulani ya Kunduchi njia ya Bahari Beach kuna mdada alikuwa amekula pombe balaa halafu alikuwa na kampani yake wadada kama wawili.

Huyo dada ambaye ndio chanzo cha ajali alikuwa anakunywa pombe, mara akawasha gari lake kwamba anaondoka kumbe alikuwa kashakolea na kitu cha alcohol. Ile anawasha gari aondoke si ikamshinda bana, acha avamie kwenye hiyo pub alokuwa anakunywa paaap ikaenda ikagonga mlango wa vioo. Bahati nzuri kulikuwa na ukuta nyuma ya hivyo vyoo gari ikaenda ikajibamiza kwenye ule ukuta ulio nyuma ya mlango wa vioo huyo mdada aliyekuwa anataka kuondoka akajibamiza kwenye kioo cha mbele cha gari yake amefumuka mdomo damu kama zote.

Nimeshangaa sana watu waliokuwa naye na wao wana magari yao pia lakini hawakumsaidia huyo mwenzao, mara paap nikatimba maana nilikuwa maeneo hayo nachukua kitimoto. Nikafika eneo la tukio fasta nakuta umati wa watu umemzunguka wanaogopa kumbeba kumuingiza kwenye gari ili akapewe matibabu, nikajikuta huruma imenishika ghafla.

Yule dada japo ni chibonge yaani huwezi amini nimevimba mwenyewe nikambeba wanaume wa Dar wamesimama tu wananishangaa. Nikaelekezwa gari ya kumuingiza yaani nimemuingiza ndani ya gari ilikuwa Prado nyeupe nashangaa hao wenzie walioshindwa kumsaidia mwenzao kipindi yupo anavuja damu pale chini, mara woote wanakuja kwenye gari kujiliza halafu wengine wakarudi pub kuendelea na wimbo unaitwa Uno.

Jamani, unapokuta janga sehemu saidia kuokoa, acheni ubaguzi na roho mbaya. Wewe dada, ugua pole umenipaka damu zako kwenye mavazi yangu hii yote kukusaidia baada ya uliokuwa nao kukuogopa kwa hali uliyokuwa nayo.
 
Sikushauri kukwepa kuwasaidia watu kwenye ajali lakini wakati mwingine kuwa makini usiguse damu za watu ovyo kuna homa ya ini (Hepatitis) na HIV.

Hiyo homa ya ini ni hatari sio lazima na wewe uwe na jeraha au mchubuko kama HIV kuweza kuambukizwa, ukiigusa tu damu ya mgonjwa imooo!
 
Asante mkuu
Sikushauri kukwepa kuwasaidia watu kwenye ajali lakini wakati mwingine kuwa makini usiguse damu za watu ovyo kuna homa ya ini (Hepatitis) na HIV.

Hiyo homa ya ini ni hatari sio lazima na wewe uwe na jeraha au mchubuko kama HIV kuweza kuambukizwa, ukiigusa tu damu ya mgonjwa imooo!
 
Kabisa maake zile damu zilikua zinatokea puani na mdomon hata kuvuta hewa ikawa ni tatizo ikabidi nichukue kitambaa nilicho kua nacho mfukoni kuanza kufuta zile damu maake zilikua nyingine zina anza kugandiana
Hao wanaume wa Dar walikuwa wanachukua tahadhari ya magonjwa, sema ubarikiwe maana bila wewe huyo dada angekata moto muda mfupi tu.
 
Hongera kiongozi. Halafu Dar es salaam kuna ushamba mmoja, mtu akipata shida ataweza mpaka kufariki, watu wanamuangalia, hakuna wa kutoa msaaada, eti wanaogopa kutoa ushahidi baadaye. Nyie wanaume wa Dar, hivi kipi bora, mtu apoteze maisha kisa unaogopa kutoa ushahidi, au bora apone then usumbuane na polisi baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom