Dada alia kwa uchungu: Bado namtafuta Mama yangu, hajulikani alipo tangu ajali ya jengo Kariakoo'

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,515
4,013
Irene Mallya anamtafuta Mama yake Happiness Mallya, mfanyabiashara wa Kariakoo mkoani Dar es Salaam, ambaye hajulikani alipo tangu ilipotokea ajali ya kuporomoka kwa jengo Jumamosi Novemba 16, 2024.

Irene amezungumza na TBC Digital katika eneo hilo la ajali Kariakoo ambapo shughuli za uokoaji zinaendelea na kusisistiza kuwa Mama yake Happiness hajapatikana hadi muda huu.

Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa

“Mama alinipigia asubuhi Jumamosi nilikuwa mbali na simu nilipokuja kupiga sikufanikiwa kuwasiliana nae nikajua tu atakuwa kwenye vikao na wafanyabiashara wenzake”. amesema Irene

Amesema baada ya hapo alipokea taarifa kutoka kwa ndugu yake aliyepigiwa simu na mama yake, lakini kwa sasa simu yake haipatikani.
 
Iweje mama na mwana wanachangia jina la BABA?

Sijaelewa hapo ila niwatakie tu pole kwa janga hilo
Mama baada ya kuolewa alienda kuongeza jina la mumewe (kwa kuapa mahakamani) ili pia lisomeke na kutambulika kama jina lake rasmi.
 
Yes kikubwa kama oxygen wanapata wanaishi, mwili wa binadamu unastahimili sana unadhoofika lakini unaishi tuombe Mungu waliobaki watolewe leo. Tuseme Amiiin
Tarehe 16, 17 leo 18. Hapo kuna tumaini kweli mkuu..??
 
Back
Top Bottom