Pre GE2025 Cyprian Musiba ashangazwa na Viongozi wa Upinzani wanaodai hakuna maendeleo kipindi cha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
1,089
2,098
Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba, ameonyesha kushangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa upinzani wanaodai kuwa hakuna maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania.

Akizungumza jijini Dodoma leo, Machi 27, 2025, Musiba amesema kauli hizo siyo tu kwamba ni za upotoshaji, bali pia zinahatarisha uelewa wa wananchi kuhusu maendeleo halisi ya nchi.

Musiba amekishauri Chama dola, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutopaswa kukaa kimya mbele ya madai kama haya, bali kinapaswa kueleza wazi mafanikio yaliyopatikana tangu utawala wa Mwalimu Julius Nyerere hadi sasa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Huu si wakati wa kukaa kimya. Wakati wapinzani wanazunguka nchi nzima wakitoa madai yao, CCM nao wanapaswa kuzunguka na kuwaeleza wananchi kilichofanyika. Wakikaa kimya, wananchi wataamini nchi haina mwelekeo," amesema Musiba.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…