CV Clinics: Msaada wa kuandika CV

Teknocrat

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
4,554
10,357
Habari wana JF

Katika harakati za kusaka ajira, au kibarua au kujitolea, katika mashirika, taasisi, kazi za serikali au makampuni binafsi , kitu muhimu kitakacho kuuza kiufanisi ni wasifu wako wa kazi au Curriculum Vitae inayojulikana kama CV yako.

Hii ndio zana muhimu yako itakayokuwezesha kutinga mguu kwenye usaili wa kazi kutokana na jinsi ulivyojieleza.

Haya hii ni fursa ya kuweka hapa muundo wa wasifu wa CV yako kutokana na elimu yako, ujuzi wako au uzoefu wako wa kazi, ili wataalamu waichambue na kukusaidia kuandika CV mujarabu kutokana na kazi unayoomba au elimu, ujuzi na uzoefu uliokuwa nao katika ombi la ajira.

*Angalizo: Hapa usiweke taarifa zako binafsi kama Jina lako halisi, Umri au anuani yako, jaribu kutumia taarifa bandia kufikisha ujumbe wa CV yako.

Karibuni waomba ajira na pia wataalamu wakuandika CV
 
Back
Top Bottom