Mbunge Afrika Mashariki
Member
- Nov 28, 2019
- 7
- 14
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MKUTANO WA HADHARA KESHO MAGOMENI KANISANI:
Mwenyekiti wa CUF-Chama Cha Wananchi Prof. Ibrahim Lipumba kesho Jumamosi Februari 11, 2023 anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye Mkutano Mkubwa wa Hadhara ulioandaliwa na Wilaya ya Kinondoni, utakaofanyika maeneo ya Magomeni Stand (Kanisani).
Katika mkutano huo utakaoanza rasmi kuanzia saa nane mchana na kutanguliwa na burudani mbalimbali, Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba atafafanua Itikadi na Sera za CUF- Chama Cha Wananchi zinazolenga kumkomboa mtanzania kutokana na Umaskini sugu wa kujitakia na kuifikisha nchi kwenye Utajirisho kupitia Rasilimali Asilia za nchi yetu na kuwafikisha Watanzania katika Haki Sawa na Furaha kwa Wote. Aidha Mwenyekiti anatarajiwa pia kuyachambua masuala mbalimbali yanayohusu taifa letu katika kipindi hiki cha ugumu wa maisha na kubainisha suluhisho.
Usipange kukosa mkutano huu muhimu.
HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!
Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Februari 10, 2023