CONTEMPORARY HOUSE- Bati gani zinafaa kuezekea.

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,757
10,479
Nimekuwa nikitamani kujenga hizi nyumba lakini changamoto imekuwa ni kuvuja.

Watu wengi naona wanapata tabu nyumba kuvuja pembeni, katikati na pale bati zinapochoka.

Kwa maeneo ya unyevunyevu kama pwani bati zinachoka ndani ya miaka mitatu tu zinaanza kuvuja. Hii ni kwa sababu Contemporary basi zake hazina slope kali hivyo huhifadhi unyevunyevu na kupelekea kuoza mapema.

Msaada wenu tafadhari.
 
1.Ezeka kwa bati za kawaida, yaani Corrugated Iron Sheets (CIS).Aidha, tumia bati zenye viwango bora vya utengenezwaji wake. Mathalani, tumia bati zilizotengenezwa kwa madini ya zinc ya kutosha, e.g. mabati ya kampuni ya Alaf Simba Dumu (kwa Tz kidogo imara).Zinc inasaidia sana kuzuia kutu.
2. Tumia mabati yenye unene (thickness) nzuri, e.g. mabati ya 28 Gauge, na kwenda juu, usitumie mabati ya 30Gauge au 32gauge ambayo ni laini sana.
3.Mtumie fundi mzuri ktk kazi hiyo, bad workmanship katika uezekaji inaweza kuwa chanzo cha kuvuja kwa paa.
4. Nyumba bora na Paa bora lililo imara linaanzia katika hatua ya awali kabisa ya "Building Plan", hivyo Plan nzuri ya jengo lazima itazaa Plan nzuri ya nyumba na Plan nzuri ya paa (roof). Tumia wataalamu ktk hatua zote za ujenzi kuanzia na hatua ya Urasimu wa Ramani za Jengo (Architectural Drawings)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom