Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,466
- 3,637
Habari Wakuu,
Mada yahusika hapo juu. Sina sababu ya kurudia kufafanua hayo maneno hapo juu ila kuna kitu ninewaza baada ya kupitia post moja ya mdau. Hizo variable anazo binadamu, ila instinct/silika ni kwa kiasi. Hayawani ndio wana hii silika kwa kiasi kikubwa kabisa. Ukiniambia wana akilli nitakataa. Labda ningewasikia wakiongea ndipo niwapime.
Hivyo kwa jinsi hayawani ukomo wao ulivyoishia kwenye silika, ndivyo kwa binadamu ukomo wao/wetu umeishia kwenye ufahamu/ consciousness. Naamini kuna lugha fulani hawa hayawani hujaribu kuongea nasi ila kwa kiasi tunawaelewa. Kwa kiasi kikubwa hatuwezi kuwaelewa.
Kwa hiyo kuna silika, ufahamu, halafu kuna ngazi nyingine ya juu yetu ambayo hatuijui na hatuiishi. Hii ndio uungu wenyewe. Inaweza pia kuwa ni ngazi moja kabla ya uungu. Sisi tunajua faida na hasara za hayawani kuwepo. Hao hayawani wanajijua? Au tunawatumia tu. Wangejua wangeendelea kuishi nasi? Leo unachinja kuku mbele ya kuku na hana wasiwasi.
Binadamu je? Katika kuwa hai kwetu tutaweza kuifikia hatua ya juu ya ufahamu tukiwa na miili hii? Tutaweza kujua faida na hasara za sisi kuwepo tukingali na miili hii? Hii hatua ya juu iliyopita ufahamu ni ipi?