Coincidence:Manchester Derby Leo April 27,2017 na Manchester Derby April 27,1974

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,274
6,592
Manchester Derby Leo April 27,2017 katika dimba la Etihad na Siku kama ya leo April 27,1974 katika dimba la Old trafford MACHESTER UNITED VS MANCHESTER CITY

Kipindi cha miaka ya 60s man united ilikuwa na wachezaji mapacha watatu ambao wa kiwango cha juu kabisa kuwahi kutokea katika ulimwengu huu wa soka.Mapacha hawa watatu walitambulika kwa majina yao yafuatayo
1.Sir Bobby Charlton-England

2.George Best(RIP)-Irish


3.Denis Law(Shujaa asiyesahaulika kamwe)-Scottish



Mapacha hawa watatu wanatambulika kama THE UNITED TRINITY kwa nyakati tofauti kila mmoja aliweza kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia .

1.Sir Bobby Charlton(alichukua Ballon dór mwaka 1966)
2.George Best (alichukua Ballon dór mwaka 1968)
3.Denis Law.(alichukua Ballon dór mwaka 1964)

Mashujaa hawa waliweza kuiongoza Manchester United kuchukua uubingwa wa ulaya(UEFA) Kwa mara ya kwanza mwaka 1968 kwa kuifunga Benfica ilitokuwa na mchezaji bora wa dunia wa mwaka 1965 Eusebio mabao 4-1.

Katika fainali ambayo Charlton alifunga magoal 2 na Best moja na lingine lilifunga na Kidd

Katika thread hii nimedhamiria kumuongelea Denis Law(Shujaa aliyeishusha timu yake daraja).
-mwishoni mwa msimu wa 1972/73 club ya manchester united ilitangaza kuwatema wachezaji wote walioonekana hawana umuhimu katika club akiwemo Denis Law.Kitu kilichomliza Denis Law kuona yeye ni shujaa aliyeitumia club kwa mafanikio makubwa toka 1962 mpaka 1972 akifukuzwa kama mbwa akiwa bado anamapenzi ya dhati ya man u.Denis Law aliitisha kikao na kocha wa manchester wakati huo Tommy Docherty

kumuomba asimuuze kwani ana mapenzi makuwa na club,without man united sitakuwa na furaha maishani(Ni maneno ya Denis Law).Haikusaidia kitu chochote katika adhima ya kocha Tommy Docherty kumtema mchezaji huyo na Denis Law kwa masikitiko makubwa akaamua kujiunga na Mahasimu wakubwa wa man united kipind hiko Manchester City katika msimu uliofuata wa 1973/74.
Msimu huu ulikuwa msimu uliokuwa na matokeo mabaya sana kwa manchester united ambapo man united walifungwa michezo 20 na kushinda michezo 10 tu.Ni msimu ambao man united waliupa jina la worst season ever huku mahasimu wao wa jadi liverpool waliuita the best moment in football history ever..
Msimu wa league 1973/74



Tommy Docherty

Mnamo tarehe 27 April,1974 ilikuwa nim mechi iliyoamua hatma ya man united kubaki au kushuka daraja,man united ilihitaji point 1 tu yaani ilihitaji sare tu ili ibaki ligi kuu ya uingereza.

Ni mechi ambayo iliwakutanisha na mahasimu wao wa jadii na majirani wa kufa na kuzikana club ya manchester city katika dimba la Old trafford maarufu kama Machinjioni kwa wakati huo.

Ni mechi iliyohudhuriwa na mashabiki 56,996(Ni mechi ya pili kuingiza mashabiki wengi katika msimu huo kwa man united baada ya ile iliyochezwa na leeds united 9 February 1974 iliyohudhuriwa na mashabiki 60,025.

Mpaka dakika ya 82 man united waliamini washafanikiwa kubaki katika ligi lakini haikuwezekana baada ya dakika ya 83 mchezaji wa Man city denis law kufunga goal la kisigino lililoitwa Backheel na kuiangamiza man united, team aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa sana.

Baada ya kufunga goal uwanja wote wa Old trafford ulikaa kimya wakiamini huo ndio mwisho wa manchester united katika ulimwengu wa soka.

Denis Law baada ya kufunga goal hilo aliamua kutoka uwanjani na kuiacha team pungufu ili kutoa mwanya mwa man united kusawazisha..Ilipofika dakika ya 85 mashabiki wa man united waliingia uwanjani na kusema mpira uishe washakubali kuwa wameshashuka daraja.

Hatimaye refa akamaliza mpira na huo ukawa mwanzo wa man united kufikilia mipango ya kupanda tena na ikafanikiwa baada msimu wa 1975/76 kurudi upya ligi kuu na hawakushuka tena mpaka leo.

(Hao sanamu watatu ni Denis Law,Bobby Charlton na George Best)




Law`s backheel


Video ya "Backheel" ya April 27,1974

By Deadbody
 
Oosshh my God. Kweli Dennis Law alionyesha mapenzi ya dhati. Ila kocha alimuumiza mno kummwaga.. GGMU
 
Mtoa mada point of correction, wachezaj hao walichukua tuzo ya mchezaj bora wa ulaya sio wa Dunia
 
Rooney hawataki kumuongeza
Kisa tu hawampendi japo kitakwimu kawafunika wotewalichomzidi ni Uchezaji bora wa dunia tu

Waingereza wanapenda kumchukia na wanachukia kumpenda Rooney.

Pamoja na mafanikio yote ndani ya klabu na timu ya taifa bado hapewi credit zake anazostahili.
Rooney ni kazaliwa katika mji ya liverpool, na ni shabiki wa everton, ni kosa kubwa sana kumjengea sanamu adui yako, nina baadhi ya marafiki zangu toka ujerumani na england ambao ni mashabiki wa manchester united, huwezi amini kitendo cha Rooney kuwa mfungaji wao bora wa muda wote kinawaumiza mnooo, ndio maana wanalazimisha Rashford awe anaanza kila mechi wakiamini kuna siku atakuja kuwa ndio mfungaji wao na si Rooney.
 
Aisee kumbe hata wazungu wanafitna na majungu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…