Mashaurijr
JF-Expert Member
- Oct 8, 2016
- 901
- 1,417
Kati ya siku ambazo sitazisahau kwenye maisha yangu yote ni leo.
Muda wa saa nne asubuhi nimeenda kutembelea biashara yangu moja mtaa fulani hapa hapa dar . Biashara ilipo lazima utumie bodaboda au bajaji kufika. Sasa ile kwenda nimeenda fresh nimefanya yaliyonipeleka mpaka saa tano na nusu.
Baada ya hapo nikatoka nikasimamisha boda nikaanza safari ya kutoka, Tumetoka mbele kidogo akapunguza mwendo ulikuwa mwendo wa kawaida tu akaniomba kuna mpenzi wake anaishi maeneo yale nyumba ipo karibu tu na barabara akaomba ampe kifuko kidogo alikuwa kaweka mbele ndio tuendelee na safari. Sikuwa na haraka nikamkubalia akaingia nyumba moja inavyumba vingi vya nje nadhani ni vyumba vya kupanga basi baada kama ya dakika tatu hazizidi tano akawa ametoka.
Akawasha pikipiki hakuniongelesha nikapanda akaanza kutoka. Njiani sasa ndio anaanza kulalamika anasema "Aisee hawa wanawake hawana shukrani kabisa, yaani kila ninachofanya haridhiki , kitu gani ambacho sijamfanyia mimi yani ananiambia nimpelekee mboga leo hana hela nimejitahidi nimemletea nakuta tayari ana mboga basi awe na shukrani ananilaumu tena mimi "
Baada ya kuongea hivyo mimi nikamwambia tu hiyo ni kawaida yao angalia usitumie nguvu zako na furaha zako zote kwa mtu ambaye haoni unachokifanya .
Sikujua kama nachochea moto huku pikipiki ikiongezwa mwendo wa hatari akilalamika "yaani sijui nimfanyie nini mimi kila ninachofanya kinakasoro Sijui nakosea wapi mimi lazima tu ile nyama kaletewa na mwanaume "
Muda huo mwendo wa kutisha najaribu kumwambia apunguze mwendo hanisikii. Hapo bado tulikuwa barabara ya vumbi mashimo mengi pikipiki inapitishwa tu. Yaani sifi tena kizembe aisee nimeponea kufa leo.
Sasa baada ya kutokea kwenye lami tu ndio imekuwa balaa zaidi yani mwendo uliokuwa unaendeshwa mpaka macho yamekauka machozi huku nikiendelea kumwomba apunguze mwendo yeye analalamika tu namwambia anishushe hasikii
Sasa kuna gari kuwa inachepuka ishawasha indicator itokoke main road yaani pale ndio ilikuwa tufie hapo jamaa kashika break zote lakini wapi pikipiki ikagonga mbele ya gari mimi urefu ukinisaidia japo nimeumia kidogo mkono una maumivu ya ndani maana baada ya kujitoa gafla nilianguka begi nililokuwa nimelivalia mbele likiniokoa nisichubuke sana ila mkono uliotangulia ndio umepata shida kidogo.
Jamaa kaumia kwenye paji la uso bodaboda wenzie fasta wamefika wamemchukua wameenda kumficha na pikipiki yake mimi nikasaidiwa na mmoja wao anayenifahamu nimekaa karibu lisaa lizima bila kuongea
Kama leo nimeponea aisee
Sitakufa kirahisi
Ndicho kilichonipata leo nikakumbuka ile video ya wale jamaa kwenye gari dereva analalamika yule mwanamke mimi nilimpa kila kitu huku akizidi kukanyaga mafuta waliopakizwa wakilia kumwomba apunguze mwendo aisee.
Aisee mapenzi ni hatari , usijiingize kijinga
Usijitoe asilimia zaidi ya 50
Hasa wakati huu wa 50/50
Kataa utumwa