Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,584
- 1,189
📍Dar es salaam
◾ 17/01/2024Habari wana-Dar es salaam. Tunamshukuru mungu kwa kutuamsha salaama siku ya leo. Wagonjwa na wanaopitia changamoto mbalimbali mungu awafanyie wepesi waweze kukabiliana nazo na kuwaponya.
➡️ Naomba tuendelee kuchukua Tahadhara katika mkoa wetu wa Dar es salaam na wilaya zote tano, kata 102 na mitaa 564.
➡️ Tujikinge na magonjwa ya mlipuko (Kipindupindu na Ugonjwa wa macho). Tuchukue tahadhari Mapema
1️⃣ Nawa mikono kabla na baada ya kula kwa maji safi sabuni au tumia vitakasa mikono.
2️⃣ Hakikisha unakula matunda masafi.
3️⃣ Chakula cha moto
4️⃣ Maji safi yaliyochemshwa na salama
5️⃣ Elimisha kuhusu magonjwa haya kuanzia ngazi ya familia yako ili kuchukua tahadhari mapema. Muelimisha mwanao kujikinga awapo shuleni na mazingira mengine
6️⃣ Elimisha jamii iliyokuzunguka kuchukua Tahadhari.
7️⃣ Kinga ni bora zaidi kuliko tiba jukumu la kujikinga na magonjwa ni letu sote na kuhakikisha tuchukue tahadhari mapema.
8️⃣ Tufuate kanuni na miongozo inayotolewa na wizara ya Afya.
⏩ Dar es salaam bila magonjwa ya milipuko inawezekana.
Nawatakia Utekelezaji mwema
UWT imara
Jeshi la mama Samia
kazi iendele
UWT ni kwa wanawake wote
Mwajabu R Mbwambo
Mwenyekiti Uwt Mkoa DSM