Chukua Hii: Mitandao ya Kijamii inatuunganisha, ila kuwa makini unapoitumia

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
334
691
Taarifa unazoweka mitandaoni haziwezi kusahaulika, hata kama umeamua kuzifuta. Hivyo, ni muhimu kuwa makini na jinsi unavyotumia mitandao ya kijamii.

Kumbuka kuwa taarifa unazochapisha zinaweza kutumiwa kuiba utambulisho wako, kufanya ulaghai, au hata kudukuliwa na kuishia mikononi mwa watu wasio salama.

Pia, ni muhimu kuwa makini na kile unachochapisha, kwani waajiri wanaweza kukufuatilia mitandaoni. Taarifa zisizofaa zinaweza kukupotezea nafasi ya ajira.

1. Picha au taarifa yako unayoweka kwenye Mitandao ya Kijamii inaweza kuishi daima, na kuiondoa haimaanishi watu hawana.

2. Zingatia kutoweka hadharani Taarifa zako Binafsi kwenye Mitandao ya Kijamii. Mfano; Kuweka Tarehe ya kuzaliwa kwenye Bios.

3. Kuwa makini unapotumia barua pepe yako. Ni vema kuwa na barua pepe tofauti na yako rasmi kwaajili ya Mitandao ya Kijamii.

4. Kama sio lazima, ni vyema kuchapisha picha zako au video za kuonesha ulikuwa sehemu fulani baada ya kuondoka eneo hilo.

Soma Pia: Jinsi unavyoweza kujilinda utumiapo mitandao ya kijamii
 
Back
Top Bottom