Itenda Jimmy Joyce
Member
- Aug 17, 2022
- 10
- 2
CHOZI la mama; Chozi hutokana na huzuni au maumivu anayoyapata mtu, inawezekana kwa sababu ya:- kusalitiwa.
-kunyanyaswa kwa aina mbali mbali.
-historia mbaya. Na mengine yanayopelekea kuhuzunisha au kuumiza moyo.
Mwanamke siyo kiumbe dhaifu kama wengi wanavyo wachukulia bali ni kwa sababu ya upole wao, unyenyekevu, uvumilivu wao na ustahimilivu wao katika mambo mbali mbali ndiyo hupelekea wengi kuamini kuwa ni dhaifu kiasi kwamba hawawezi kufanya jambo bila kutegemezwa au kusimamiwa.
Wanawake hulazimika kuvumilia mateso mengi kwa sababu maalumu kama vile:-
-kulinda heshima ya ndoa yake.
-watoto wasiteseke
-heshima wa wazazi na sabanu zinginezo. Hayo yote humtambulisha mwanamke.
Pamoja na kuwepo kwa taasisi mbali mbali zinazolinda haki za mwanamke, bado kuna nyanja moja ya unyanyasaji ambayo inapelekea mwanamke kukosa uhuru, kujiamini na kujikuta hata anaunga mkono imani potofu kuwa ni kweli yeye hawezi. Nyanja hiyo ni unyanyasaji wa KISAIKOLOJIA.
Hii inaweza kutokea kwa mwanamke aliye kwenye ndoa hata yule ambaye bado hajaingia kwenye ndoa. Na athari hizi chanzo chake huanzia katika ngazi ya familia Kwa yule ambaye bado hajaingia kwenye ndoa anaweza kuathiriwa na:
-jamii inayomzunguka. Pale wamapoamini kuwa msichana faida yake ni mahali tu inayotolewa akihitajika kuolewa na kwa kumhudumia mumewe basi.
-historia mbaya ya maisha yake, kama vile kubakwa, kufiwa wazazi, kutelekezwa Na sababu zingine mbaya.
Mwanamke huyu anaweza kukosa haki yake ya kupata elimu kwa sababu tu wazazi hawaamini juu ya uwezo wake, hivyo anaweza kukua akiambiwa kuwa wewe huwezi badala yake subiri uolewe ukamhudumie mume wako maana ndilo jukum lako pekee bila kufahamu kuwa anauwezo mwingine tofauti na kuhudumia mume pekee, jambo ambalo baada ya mume kufariki hubaki tegemezi bila msaada wowote wala fani yoyote.
UNYANYASAJI WA KISAIKOLOJIA; hutokana na maneno mabaya (hasi), kupigwa mara kwa mara au kukumbushwa mambo mabaya aliyowahi kuyapitia.
Wanawake wengi hawana uelewa juu ya aina hii ya unyanyasaji hivyo hukaa kimya hata pale inapoonekana kuwa hawatendewi haki hasa kuu katika ndoa zao. Kuna baadhi ya maneno ya huharibu saikolojia ya mwanamke ambayo anaweza kuyasikia kutoka kwa mumewe kama vile:
Wanawake wengi wamekuwa tegemezi kwa sababu ya kushindwa kujisimamia wenyewe, na kuishia kufanya vitu vidogo vidogo kwa imani ya kwamba wao ni viumbe dhaifu.
Wengi wametelekezwa na waume zao kisha kubaki na watoto wakihangaika, wengine kukosa mahitaji muhimu kama nguo, chakula na malazi.
Jambo muhimu kwa kila wanawake ni hili.
Kuamini ya kwamba kuna nguvu au uwezo wa pekee ndani yake ambao hakuna anayeweza kuuzuia au kuuzima. Pia kila mtu ana ndoto ya kufikia malengo fulani, hivyo anapaswa kutumia uwezo ambao Mungu amempa ili kutimiza ndoto zake. Haijalishi amechelewa kiasi gani, haijalishi amekatishwa tamaa mara ngapi bado uwezo wake upo.
Asubuhi ya leo haiwezi kufika bila kulivuka giza la jana hivyo yote magumu yaliyotokea ni giza lililokuwa linaikaribisha leo yako, amka upiganie ndoto zako ukipinga imani potofu.
Hivyo basi, mbali na kupigwa, kufukuzwa na mateso mengine taasisi zinazohusika na haki za wanawake zinapaswa kuangalia kwa kina nyanja hii ya unyanyasaji ambayo ni ya kisaikologia. Kwani saikolojia ndiyo huamua maamuzi gani mtu ayachukue. Wengi wananyanyasika pasipo wao kujua, hata wakijua hawajui ni wapi wakaseme maana wanaamini taasisi zipo kutetea tu wale wanaopigwa au kutelekezwa.

- Nitaoa mwanamke mwingine ubaki na wanao.
- Nitakuua
- Nitakupiga nikuumize vibaya.
- Wewe utabaki kuwa mwanamke tu hakuna unachoweza bila mimi.
- Nitaacha kukuhudumia. Na mengine ya kuvunja moyo, maneno ambayo yakisemwa mara kwa mara hupelekea mwanamke kuzoea kisha hugeuka kuwa sehemu ya maisha yake, hivyo hushindwa kutoa taarifa kwa taasisi husika maana alipoambiwa mara ya kwanza hakuona madhara yake na kwa sababu anahitaji kulinda ndoa yake alikaa kimya, mwisho wa siku hugeuka na kuwa maisha yake halisi.