China yazidi kujiimarisha kijeshi, yazindua melivita mpya

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Salaam wana JF




Serikali ya China imezidi kuliimarisha jeshi lake la majini baada ya kuzindua meli mpya aina ya 001A lakini bado haijapewa jina maalumu,melivita hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba ndege vita aina za Shenyang J-15, makombora,na vifaa vingine vya kijeshi iliobuniwa 2013 na kuanza kutengenezwa mwaka 2015 itaendelea kufanyiwa majaribio mpaka mwaka 2020 ina uwezo wa kubeba vifaa vya uzito wa tani 70000, melivita hiyo imetengenezwa nchini China kwa tekinolojia ya China inafuatia melivita nyingine ya China aina ya Liaoning ilionunuliwa miaka ya 90 kutoka Ukraine.

Hali hiyo imefuatia tishio la kiusalama kutoka Marekani katika pwani ya bahari ya kusini mwa China kitendo cha Marekani kuitishia Korea Kaskazini kijeshi, vilevile kufuatia Marekani kuweka mifumo ya kiulinzi ya makombora katika pwani ya Korea kusini inayojulikana kama THAAD, Serikali ya China na Korea kaskazini inasema inaweza kuingilia mifumo mingine ya makombora katika eneo hilo.

Uwezo huo wa kijeshi utaiwezesha serikali ya China kulinda maslahi yake ya kiuchumi hasa katika bahari ya kusini

BBC NEWS
 
Hii ndo ile wanataka kuiita Shangdong nadhani...
Itakua ya pili kwenye Aircraft carriers za PLA Navy
 
Wataalamu wameshangazwa na kasi ya utengenezaji kwa hii manowari....Kwa maana km meli vita za destroyer au frigate zenye uzito kuanzia 1500Tone hadi 12,000Tone zimekua zikichukua hadi muda wa miaka 2 hadi 5 hadi kukamilika kwake sasa ndo iwe kwenye Aircraft carrier km hii yenye massive tonnage zaidi ya 50,000Ton kwakweli ni kasi ya ajabu sana maana hili dude sie tunaliona kwa picha apo ila ni Gigantic yani ni dude kubwa sana ambalo ndege vita,Helicopter na vigali vya kuvutia ndege vinakua juu yake.....Kwa uweoz huu Ina maana ndani ya miaka 10 na kwa uwezo wa kifedha wa sasa wa China inauwezo wa kumiliki hizi Manowari kuanzia 6
 
Tuliwahi letewa humu video ikionyesha wachina kwa bidii sana walimaliza kujenga ghorofa leefu sana kwa kupindi kifupi sana. Nimesahau ulikuwa ni muda gani ila ulikuwa mfupi wa kustajabisha sana. Wachina ni siafu shambulia shambulia.
 

Mkuu labda wametumia 3D Printers (utani) kuhunda Carrier zao in a recordtime - kama wanaweza kujenga nyumba za kufikia ghorofa kumi kwa kutumia 3D printers kwa nini tushangae ya kuhunda Meli? Wachina ni binadamu resourceful sana - wanaweza kutumia composite material badala ya steel na alloys nyingine, remember there are some composite material ambazo ni harder kuliko steel.
 
Tuliwahi letewa humu video ikionyesha wachina kwa bidii sana walimaliza kujenga ghorofa leefu sana kwa kupindi kifupi sana. Nimesahau ulikuwa ni muda gani ila ulikuwa mfupi wa kustajabisha sana. Wachina ni siafu shambulia shambulia.
walijenga kwa siku 3.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…