China yapinga ujio wa meli ya kisasa yenye teknolojia ya hali ya juu ya jeshi la Marekani

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,417
9,603
China imepinga vikali ujio wa meli ya kisasa yenye teknolojia ya hali ya juu kabisa ya jeshi la Marekani-- USS Zumwalt(DDG-1000) ambayo inatarajia kuzuru pwani ya Korea karibu na China.
Jeshi la maji la Marekani mapema mwaka huu lilitangaza kwa Mara ya kwanza ziara ya USS Zumwalt kwenye bahari ya Japan au bahari ya mashariki ndani ya mwaka huu.
China imesema kwamba inatazama ujio huo wa USS Zumwalt kwa karibu sana.
Wizara ya mambo ya Nje ya China imekosoa ujio huo na kuonya njia zozote za kuhatarisha usalama wa Uchina na kuonya kwamba nchi zote zinazohatarishiwa usalama zinapaswa kushirikiana pamoja kijeshi ili kuepusha mivutano na kulinda amani na usalama.
USS Zumwalt ni meli ya kisasa yenye teknolojia ya hali ya juu kabisa ya ikiwemo kupunguza uwezo wa kuonekana kwenye rada(stealth).Ina uzito wa tani 15000 na pia ina uwezo wa kutungua makombora ya ballistika kwa kutumia mifumo ya kisasa kabisa ya kutungua makombora ambayo ni SM-1,SM-2 na ule wa kisasa zaid wa SM-6.
Ujio huo wa USS Zumwalt unakuja ikiwa kama juhudi za Marekani kuonyesha na kudumisha ushirikiano na washirika wake ikiwemo Japan na South Korea dhidi ya Korea kaskazin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…