Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 725
- 1,458
We si ulikua unasikia TU mtandao wenye kasi ya 5G, 6G sasa China wametambulisha mtandao wa intaneti wenye Kasi balaa wa 10G.
China imezindua mtandao wa kwanza wenye Kasi Duniani wa kibiashara wa 10G broadband mjini Xiong'an, uliotengenezwa na Kampuni ya Huawei pamoja na China unicom.
Huu ni Mtandao wa kizazi kijacho (next generation internet) yenye spidi Kasi ya 9,834mbps kufanikiwa kuweka alama mpya ya kimataifa. Ina uwezo wa kupakua movie yenye ukubwa 8k video kwa sekunde moja TU.
Kama china watafanikiwa kusambaza mtandao huu basi miji mbalimbali kama vile Shanghai , Beijing, Shenzhen na Guangzhou wataweza kupata huu mtandao na kusaidia kwenye Maendeleo makubwa ya Teknolojia na miundombinu kwa kurahisisha maisha.