China-US (TechWar): China limekuwa taifa la kwanza duniani kufanikiwa majaribio ya 6G, likiitangulia Marekani na washirika wake

Xi Jinping

JF-Expert Member
Jun 14, 2023
1,996
6,355
Kwenye mbio za nani atatangulia kwenye teknolojia ya mawasiliano ya 6G ilikuwa ni race kati ya China na Marekani na washirika wake.

China ilikuwa imeshajiwekea mkakati wa kuifanyia tafiti teknolojia ya 6G hivyo ikawa moja ya kipaumbele cha taifa kwenye mpango wa miaka 5 ulioitwa China's Fourteenth Five-Year Plan (2021-2025)

February 2024, Marekani kama kawaida bila kuishirikisha China wakaanzisha '6G alliance' na mataifa ya Australia, Canada, Czech Republic, Finland, France, Japan, South Korea, Sweden na U.K kwa ajili ya 6G.

Wakijua kuwa huenda China itatangulia kudevelop tech ya 6G kabla yao, mataifa hayo yakiongozwa na Marekani February, 2024 yakaweka principal ya 6G wakisema:
  • The next-gen wireless networks (6G) are developed with ‘trusted technology that is protective of national security’
Lengo ni kwamba China ikitangulia waseme kuwa teknolojia ya China ya 6G haimaniki kwa usalama wa taifa litakaloitumia.

Hilo halishangazi kwenye China-US tech war kwa sababu mwaka 2019 serikali ya Marekani ilisema kuwa HUAWEI na ZTE ni hatari kwa usalama wa taifa kwamba zinatumiwa na serikali ya China kukusanya taarifa. Safari hii wameamua kujihami mapema kwa kuweka principa fake. Vita ya teknolojia ni ngumu sana kwa ground.

Wakati muungano wa mataifa wakiendelea kupambana kufanyia tafiti 6G na kuweka principal kwa teknolojia ambayo bado hawajaizundua hata kuifanyia majaribio, kwa upande wa China wameweza kufanikiwa kufanya majaribio ya kwanza duniani ya 6G mnamo 10 July 2024.


Hilo liliwezekanaje?
  • Baada ya tafiti za miaka kadhaa hatimaye kundi la wahandisi wa mawasiliano ya simu wa China likiongozwa na academician, Prof. Zhang Ping wa Beijing University of Post and Telecommunication wakaanzisha mtandao wa kwanza wa majaribio duniani wa mawasiliano ya 6G. (The world's first field test network for 6G networks)

Kwa kutumia vipimo maalumu vya mawasiliano, majaribio hayo yameonyesha kuwa 6G imekuwa na ubora mara kumi ukilinganisha na 5G. Hii ni katika key communication metrics, capacity, coverage and efficiency.

Pia, habari njema ni kwamba mtandao wa majaribio umeonyesha kuwa inawezekana huduma za 6G kufanyika katika miundombinu iliyopo ya 4G na 5G.

Baada ya majaribio hayo mpango uliopo sasa ni kuifanya teknolojia ya 6G kuwa ya kibiashara kufikia 2030. Yaani teknolojia hiyo ianze kutumika kwenye vifaa vya mawasiliano, huku viwango (standards) za 6G vikitarajiwa kuwekwa mnamo 2025.


Je, Marekani haijajifunza?

  • Mwaka 2011 Marekani ikishirikiana na mataifa mengine iliizuia China isijiunge kwenye kituo cha kimataifa cha anga za juu, International Space Station (ISS). Mwaka 2022 China wakafanikiwa kuanzisha rasmi kituo chao cha anga za juu kiitwacho Tiangong Space Station (TSS) na kufanya viwe viwili tu katika anga za juu, cha Kimataifa (ISS) na cha China (TSS)

"No one can contain China or stop its development.”
Alexander Lukashenko (Belarus president)
 
Marekani umtishie na Mambo sijui 5g, 6g. Mambo hayo mbona madogo sana. Misingi ipo utamtishaje mmarekani.
 
Marekani umtishie na Mambo sijui 5g, 6g. Mambo hayo mbona madogo sana. Misingi ipo utamtishaje mmarekani.
Telecommunications ni biashara ambayo inaingizia taifa mapato.

Leo hii ukienda Germany 50% ya mifumo ya telecommunication wanatumia vifaa vya 5G vya HUAWEI na ZTE.

Hiyo ni Germany peke yake haujagusa nchi zingine za Ulaya, Marekani yenyewe na worldwide. Unafikiri serikali ya China na hayo makampuni yanaingiza kiasi gani cha pesa kwenye uchumi wao?

Huawei na ZTE kwa pamoja ni kampuni za China ambazo zinauza sana vifaa vya mawasiliano vya 5G kuliko kampuni za West kama Nokia, Siemens na Ericson. Kwa ujumla zinashare global market karibu 50%

Watakapotangulia tena kuingia kwenye global market na 6G ina maana watazidi kujiimarisha na kuongeza mapato

Kwenye global market Marekani amepigwa gap kwa mbali sana na China kwenye telecom tech ndio maana anaomba ushirikiano na mataifa mengine ili ku-compete na China

Ingekuwa Marekani hatishiki na ni vitu vidogo kwake asingehangaika kiasi hicho
 
Back
Top Bottom