China kujenga viwanda 200 vitakavyotoa ajira kwa watu 200,000

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Waziri mambo ya nje China kufanya ziara Tanzania Januari 09, 2017 atajadili mpango wa uendelezaji wa viwanda ambapo China itajenga viwanda 200 kabla 2020.

Mbali na hayo ziara ya waziri mambo ya nje wa China nchini pia italenga kujadili miradi kadha wakadha ya maendeleo kama ifuatavyo;

1. Maboresho reli ya TAZARA
2. Ujenzi bandari ya Bagamoyo
3. Ujenzi reli ya kati



Hayo yalibainishwa jana na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya kikazi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi.

Waziri Yi anatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi ijayo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara hiyo, Mindi Kasiga, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa ziara hiyo imelenga kukuza uhusiano kati ya China na Tanzania na kuangalia maeneo mapya ya kiuchumi.

Alisema viwanda vitakavyoanzishwa na Wachina nchini vitagusa maeneo yote muhimu ikiwamo sekta ya kilimo.
 
mbona nlisikia bandari ya bagamoyo imeota nyasi kwenye mipango, then kama ndo hvyo hz ndo fununu za kudhibitisha uwekaji wa vikwazo kwa wamerekani juu yetu! "lala na fegi uchome kibanda uwiii wacha maneno weka muziki uwiii!"
 
Ndo vile viwanda mpaka vingine vya kukaanga karanga na kuchemsha mayai?
 
Nyie mlisha onaga watanzania mbumbumbu kweli. Yani waziri wa china ajenge viwanda nchi nyingine kwa faida ya nchi yake au Tanzania?
 
acha ujinga wewe wakujengee viwanda. kwa Sera na mkakati gammo ulionao?? Umeme shida

malighafi shida. aridhi haijapangwa kussuport viwanda
mwambie magu ajipamge sana kama kweli anamaanisha viwanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…