Chile: Mji mzima wateketea Kwa Moto, tusipuuze Manabii

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,382
31,995
Salaam,Shalom,

Wiki mbili zimepita sasa, iliripotiwa mlipuko mkubwa wa moto Kutoka msituni uliosambaa na kuteketeza mji mzima. Watu wengi wamefariki, nyumba za mji huo kugeuka majivu kabisa,Chanzo Cha moto huo hakijafahamika Hadi sasa,ingawa mamlaka zinasema chanzo, yaweza kuwa ni ARSON!!!

Jinsi mji huo ulivyoteketea, Si Rahisi kuamini moto Kutoka msitu wa asili ndio chanzo Cha kuteketea kwake. Yaani ni kama vile mtu alichukua kiberiti na kiteketeza mji Kwa petroli, mji mzima ni majivu!!

Kumekuwa na ujumbe unaojirudia wa Manabii wa Mungu kuwaarifu wakazi wa Bandari salama kuhama mji huo, watu hawataki kusikia sauti ya manabii wa Mungu.

Utii ni Bora kuliko SADAKA.

Source: ALJAZEERA TV.
 
Nabii anahusikaje hapo !! Moto una visababishi watakuja na report jinsi moto ulivyotokea ! Na kilichosababisha

Mnawapa kichwa sana hawa watu na story za unabii !! Hiyo alibahatisha tu mkeka umetiki anaenda kukamata watu akili hapo!

Kama alitabiri kwamba moto utatokea kwanini asiombe akazuia. Au ndo mnataka kusema Mungu anashindana na watu anaojua kabisa anawazidi uwezo.

Anaona kabisa hivi ni viumbe dhaifu bado anavionesha mabavu kwa maumivu.

Anaumba watu halafu anawateketeza kwa moto for what? Kwanini asiwaoneshe upendo wakazidi kumuamini sio kwa vitisho na adhabu?
 
Nia ya thread ni kuwaarifu waaminio kuchukua hatua,

Wabishi endeleeni kusubiri.
Huwezi kuamini ujinga then uchukue hatua hayo ni matumizi mabaya ya Imani.

Maana Imani ni kuchukua hatua ya kile unachokiamini
Ukiamini vibaya utavuna mabaya ukiamini vema utavuna mema.

Walokole mpo na problemas za kuamini taarifa mbaya badala mtumie Neno kugeuza mabaya kua Mema.

But you dudes mnajaribu kusaport evils!
Non sense!
 
Back
Top Bottom