Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,017
- 1,985
Chifu Anthony Thadeo Wangao, Chifu Kapufi wa Tatu wa Sumbawanga Asilia, ametoa kauli yenye uzito kuhusu baadhi ya watu wanaopinga mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Akiwa kiongozi wa kimila anayeheshimika sana katika Mkoa wa Rukwa, amesema wazi kuwa watu wanaopinga uchaguzi ni wale ambao hawakujitokeza kujiandikisha wakati wa zoezi rasmi la kitaifa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema wananchi wote wa Sumbawanga walipata fursa sawa ya kujiandikisha, hivyo wanaopinga uchaguzi sasa ni wale wanaoogopa kushindwa kwa aibu, kwa kuwa hawana uwezo wa kushindana kisiasa wala hoja za msingi. Chifu Wangao amewataka wananchi wapuuze kelele za kisiasa kutoka kwa wanasiasa waliokosa sera na mwelekeo.