Chenge na Ngeleja kuongoza kamati ya sheria ndogo ya Bunge, najifunza haya

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
746
635
Leo taarifa imetoka juu ya kuundwa kwa kamati mbalimbali za Bunge za mwaka 2018-2020. Ni kawaida kwa uwepo wa kamati hizi, kwani zimekuwa zikisaidia mambo anuai yenye maslahi mapana kwa taifa. Kwa mfano, mwaka 2014, kamati ya Bunge ndiyo iliwatendea haki wananchi juu ya kufichua maovu ya Tegeta ESCROW, ingawa hadi leo hatujui linavyopelekwa na wala hatun uhakika kama hela zetu za bia saba saba kama wanamahesabu walivyokuwa wakitupigia hesabu. Badala yake wamebaki kuweka vyambo tu vya kafara.

Kati ya kamati kadhaa za Bunge, kuna hii kamati ya sheria ndogo. Mwenyekiti wa kamati hii ni Bw. Andrew Chenge na makamu wake ni Bw. Williamu Ngeleja.

Sasa hapa tunapata picha gani Watanzania? Andrew Chenge yupo kwenye tuhuma kibao ikiwemo na za ununuzi wa RADAR, RICHMOND na TEGETA ESCROW. Williamu Ngeleja yupo pia kwenye tuhuma nyingi za ufisadi, na kwenye moja ya tuhuma zake, ipo hii ya Tegeta ESCROW kupewa gawio na Singasinga. Na kwa kuthi-bitisha hili, kwa mikono na miguu yake mwenyewe, baada ya kuona wananchi wamemkalia kooni, akaamua kuzirudisha ili kujinasua. Hajawahi kuchukuliwa hatua hadi siku hiyo.

Nini maana ya watu hawa kuongoza kamati ya Bunge ya sheria ndogo?

  1. Yawezekana serikali imemtumia Ndugai kuwaweka watu hawa ili kupindish sheria zinazoonekana vikwazo kwa watawala wa awamu hii. Tukumbuke kuwa, Chenge ni nguli wa sheria.
  2. Vilevile inawezekana ni mpango mahususi wa kuwaweka watu hawa ili suala la kuongeza muda wa rais kukaa madarakani. Isisahaulike kuwa, Nkamia alirejesha hoja yake binafsi ya kutaka hili lipite, na kwa sasa kawekwa kwenye moja ya kamati za Bunge.
  3. Yawezekana ni kujaribu kuwafutia kabisa tuhuma watu hawa waliwahi kukutwa na Bunge wakiwa nazo ikiwemo kwenye kashfa ya Tegeta ESCROW, RICHMOND na ununuzi haramu wa kifaa kibovu cha RADAR?
  4. Je, yawezekana Ndugai ameamua kutumika kisawasawa ili kuhakikisha upinzani unakosa nguvu Bungeni?
  5. Je, inawezekana ukawa mpango mahsusi wa kuimarisha ngome ya CCM kwenye kupitisha miswaada mibovu ambayo upinzani umekuwa ukizipigia kelele?
Watanzania, uwepo wa watu hawa wawili kwenye kamati ya Bunge ya sheria ndogo ni kielelezo tosha kabisa kuwa, hoja binafsi ya kuongeza muda wa rais kusalia madarakani utapitishwa kwa msaada mkubwa sana wa watu hawa wawili, na tusisahau kuwa wanao ushawishi mkubwa kwa wabunge wenzao.

Ushauri wangu. Wabunge wanaopenda uhai wa taifa hili, ipo haja kuliona hili na kuchukua hatua ili kuwaondosha mapema kabisa watu hawa wawili ili wasishike nafasi yoyote ile ndani ya Bunge. Ikiwezekana, hata uenyekiti wa Chenge uangaliwe upya, najua Bunge kwa umoja wake, linao uwezo wa kuwaondosha mapema na haraka iwezekanavyo. Tunahitaji Tanzania ya Watanzania, siyo Tanzania ya Chenge!

Uncle Kaso
13.03.2018
 
Chenge ndiye mwanasheria bora kabisa kuwahi kutokea hapa Tanzania ambaye amewahi kutuhumiwa tu bila kushtakiwa popote!
 
Jamaa baada ya kuona wananchi wanamchenjia kaona bora awaombe poo watuhumiwa wa ufisadi ili wamsaidie kupitisha ajenda zake na kuwabana wapinzani pia kutupilia mbali hoja ya Bashe inayopigiwa debe na Nape & co pamoja na wapinzani.
 
Sasa hapa nawaza ikitoka amri toka juu ya kuwaondoa Chenge na Ngeleja kwenye hiyo kamati si itakuwa uhuru wa muhimili wa bunge unaingiliwa?
Au sasa tukubaliane kwamba wakati fulani lazima mihimili iingiliwe na mhimili mkuu kuokoa nchi yetu?

Assuming uteuzi wao sio amri toka juu.
 
Back
Top Bottom