Mimi naamini kabisa kama Mh.Kikwete ni msafi tena msafi wa uhakika.kama kuna wachafu basi hao walidandia basi la Mh.Kikwete na kutaka kumsaidia wakiweka matumaini kuwa atawapatia lifti ,mara nyingi wanaosaidia kusukuma gari nao hutaka msaada wa kufikishwa wendapo.
Kwa ufupi Mh.Kikwete hakuwa mwizi wa fadhila aliwapa msaada na kuwafikisha waendapo ,kama walikula dawa ili wapate nguvu za kumsaidia hilo litakuwa tatizo lao ,Mh.Kikwete hakutaka kujua jamaa walipata wapi nguvu za kulisukuma gurudumu lake la kupanda kilima cha Uraisi kwa kishindo ,yeye aliona tu kuwa gari limeshika kasi na kuondoka hivyo aliowapakia aliwasaidia kwa kuwalipa shukurani.Sasa kusema Kikwete alishinda kwa sababu wasukumaji wake walikula vidonge vya kuongezea nguvu ili waweze kulisukuma gurudumu na wao wapatiwe lifti ,hilo litawagusa hao waliotumia vidonge si kwa msukumwaji.Kawafikisha safari yao ,sasa kama waliiba fedha za kupata nguvu au hapo walipofikishwa ndipo walipokusudia kuiba ,that will be another case ,fagio la chuma likipitishwa inavyotakiwa Mh.Kikwete asiukumbuke ule wema aliotendewa kwani alikwisha walipa wema ,atimize majukumu ya Uraisi na kuangalia mbele awache sheria ichukue mkondo wake huku yeye akiwa msimamizi na kuwaeleza wasaidizi waliomsaidia kusukuma gurudumu kuwa kama angelijua ni majambazi asingeliwafikisha safari yao.