Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,535
- 1,178
Chato Samia Cup yasaini mkataba wa ushirikiano na Suluhu Academy ya Kizimkazi Zanzibar
Tukio Hilo limefanyika Wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya chato Samia cup 2024 iliofanyika kwenye Uwanja wa mazaina uliopo chato mjini kati ya Timu ya mashabiki wa Simba wilayani Chato Dhidi ya Suluhu sports academy.
Tukio hilo pia limeshuhudiwa na Mhandisi Deusdedith Katwale Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya Chato Samia Cup ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora. Akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa geita Mhe: Martin shigella, mkuu wa Wilaya ya Geita mjin Mhe Hashim Abdallah komba amewaasa viongozi na Wadau wa Michezo wilayani Chato Kutumia Fursa hiyo kuonyesha ushirikiano Ili kuendelealza michezo Kwani ni Moja ya jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta Ya Michezo Nchini.
Aidha Komba amewata viongozi hao kuacha kuihusisha chato Samia cup na hisia nyingine ..
"Vipaji vinavyoibuliiwa hapa ni Kwa faida chato,mkoa na Taifa Kwa ujumla ,oneni Dhamira njema ya chato Samia cup na isiwekewe hisia hisia nyingine maaana ni kukwamisha vipaji vilivyopo kwenye maeneo yenu,turuhusu shughuli za maendeleo zifanyike badala ya kuweka hofu na Kutaka kukwamisha" Mhe Kombe Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Soma Pia: Samia Cup Kuinua Vipaji Same
Naye katibu wa Chama Cha soka wilayani Chato (CDFA)Wilfred Machugu ambaye ameshiriki zoezi la kusaini mkataba Amekiri Kuwa mkataba huo ni msaada mkubwa Kwa chama Cha soka pamoja na wadau wa Michezo Kwani itawasaidia kuwaendeleza vijana waowapata kupitia Ligi ya chato Samia cup na Mashindano mengine kuwapeleka kwenye kitua Cha micheza Cha Suluhu academy kwaajili ya kujiendeleza Zaidi.
Kwa Upande wao Baadhi ya Wachezaji kutoka wilayani Chato wameishukurua Taasisi ya chato Samia cup Kwa kuwaleta Suluhu sports academy wilayani hapo Kwani hatua hiyo imeongezea hamasa ya vijana kuonyesha uwezo wao Ili waweze kuonekana na kuendelezwa zaidi .
Zoezi la kusaini mkataba huo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na kisiasa akiwemo mwazilishi wa Ligi ya chato Samia cup Deusdedith katwale ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini..
Huu ni msimu wa pili wa Ligi ya chato Samia cup kufanyika ambapo Baada ya uzinduzi huo Ligi hiyo itaendelea Kwa ngazi ya Chini kuanzia vijijini ambapo Zaid ya Timu 100 zinatarajiwa kushiriki Ili kumpa Bingwa ambaye atajinyakulia kombe na zawadi ya Shilingi million mbili .