Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,618
- 1,198
Chatanda Ataka 20% ya Wagombea Nchini Wawe Wanawake
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, amesema kutokana na hali ilivyo wanataka asilimia 20 ya wagombea wa majimbo, udiwani na serikali za mitaa wawe wanawake hasa katika uchaguzi ujao.
Chatanda amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa uliowashirikisha wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Mkutano huo ambao lengo lake ni kufanyia kazi msimamo wa Rais Samia katika kuleta umoja wa kitaifa kwa kudumisha maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya umoja wa kitaifa kwa vitendo.