Chatanda afungua semina ya viongozi wa UWT mkoani Shinyanga, ahimiza wanawake kuwania nafasi za uongozi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,069
716
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Ndg. Mary Chatanda akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Taifa, tarehe 01 Julai, 2024 amefungua Mafunzo ya usambazaji wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022 Kwa viongozi na watendaji wa Makundi maalum Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambayo yameandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Santiel Eric Kirumba.

Mhe. Chatanda ametumia adhira hiyo kuhimiza Wanawake wenye uwezo na sifa za uongozi kujitokeza kuwania uongozi Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa Kufanyika Novemba 2024 ili kujaza nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa, Kijiji na vitongoji na wajumbe wao.

Kadharika amewakumbusha Wanawake na Wananchi kujitokeza Julai 20, 2024 kujiandikisha kwenye daftari la Makazi pamoja na Mpiga Kura ili kujiandaa vyema kushiriki katika uchaguzi wa serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu 2025.

IMG-20240702-WA0082.jpg
IMG-20240702-WA0077.jpg
IMG-20240702-WA0074.jpg
IMG-20240702-WA0075.jpg
IMG-20240702-WA0076.jpg
 
Back
Top Bottom