SoC03 Chanzo cha malalamiko juu ya mfumo wa kodi, suluhu ni lipi ili kuhamasisha walipa kodi

Stories of Change - 2023 Competition

Mary Abely

New Member
Jun 15, 2023
4
4
UTANGULIZI
Kodi ni muhimu kwa kila mwananchi, kwa maana hutoweza kuiwajibisha serikali kama hulipi kodi. Pia ni muhimu kulipa kodi ili kupata huduma bora kama elimu, ulinzi, afya na miundombinu. Mbali na umuhimu wa kulipa kodi, Tanzania imekua ikikumbwa na malalamiko juu ya juu ya sheria tofauti za kodi na tozo mbali mbali kwenye huduma. Pia, wananchi wamekuwa na malalamiko juu ya utelekezwaji wa sheria za kodi na mamlaka husika.
Malalamiko hayo ni pamoja na;
  • Kodi haziakisi hali halisi ya sasa ya kijamii na kiuchumi,
  • Taratibu za kulipa kodi ni ngumu na huleta usumbufu,
  • Gharama zinazoambatana na utekelezaji wake ni kubwa ,
  • Usimamizi wa kodi hauko wazi na hautoi haki ya kutosha na rufaa ya kodi haipatikani kwa walipa kodi wengi.
Sababu hizi zimechangia kupunguza wigo wa kodi na utekelezaji kuwa duni. Kwamfano, mwaka 2017 Wizara ya fedha na mipango imeonyesha kuwa jumla ya biashara 1872 zilizopo Dar es salaam na Arusha zimefungwa, kaodi ikionekana ndio sababu ya kuu ya biashara kufungwa.

Nchi yetu ya Tanzania inakumbwa pia na tatizo la watu kukwepa kulipa kodi, licha ya kuufahamu ukweli juu ya umuhimu wa kulipa kodi na madhara ya kutolipa kodi. Kwa mfano Ripoti ya ISCEJIC 2017, inakadiria kuwa nchi huwa inapoteza Tsh billion 4,090 kwa mwaka katika mapato kutokana na vivutio vya kodi vilivyotolewa ikiwa; uhamishaji wa mtaji haramu, utakatishaji wa fedha, kuacha kutoa risiti kwa mauzo, na makampuni makubwa kubadili majina ya kampuni ili kukwepa kulipa kodi.

yafuatayo ni mapendekezo ambayo yanaweza kusababisha kuanzishwa kwa mfumo endelevu unaomlenga mlipa kodi , unaofata haki na usawa, ambao utapelekea uwezekano wa kupanua wigo wa kodi na kuhamasisha wanachi kulipa kodi.

Kwanza, Njia za ukusanyaji kodi ziwe rafiki, mbinu kama kufunga akaunti za wafanya biashara, kunyang'anywa mashine za EFD, kutishiwa kufunga biashara hukatisha tamaa walipa kodi hivyo, hukwepwa kulipa kodi. kuna umuhimu wa wa kufuata sheria, haki za mlipa kodi kama kuaminiwa, faragha na usiri, na kutumia njia nyingine za kuhamasisha watu kulipa kodi bila vitisho. (chanzo: TRA haki za mlipa kodi).

Pili, Kuimarisha njia za kupambana na rushwa, rushwa hudhofisha utawala bora na hondoa uaminifu wa wananchi kwenye mfumo wa kodi. Njia madhubuti ni muhimu ili kudumisha uadilifu na uwajibikaji. Tanzania iboreshe mifumo ya kuchunguza na kugundua rushwa kwenye usimamizi wa kodi, hii inajumuisha, kuimarisha udhibiti wa ndani ya mfumo, kuwalinda watoa taarifa za rushwa, na kutoa adhabu kali za vtendo vya rushwa.

Tatu, kuongeza utoaji wa elimu kwa walipa kodi ili kuwahamasisha watu juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kupunguza ukwepaji wa kulipa kodi. Inabidi kuwekeza kwenye kwenye kampeni za kutoa elimu kuhusu kodi, semina na kutumia mitandao kusaidia walipa kodi kujua haki na wajibu wao.

Nne, kuimarisha mifumo ya usuluhishi wa migogoro. Hii inajumuisha kuondoa vikwazo katika mifumo ya usuluhishi wa migogoro ya kodi. Kwamfano, mfumo wa Tanzania wa rufaa ya kodi, unamtaka anaebishia kodi kuhusu makadirio anatakiwa kulipa 1/3 ya kodi anayobishia kabla ya pingamizi lake kukubaliwa.( chanzo: Sheria ya usimamizi wa kodi 2015).

Mwisho.
Kodi ni moja ya kigezo kitumikacho na wananchi kuiwajibisha serikali yao, hasa katika ubora ubora wahuduma za kijamii. Watanzania wengi wanashindwa kutambua umuhimu uliopo juu ya ulipaji wa kodi. Sambamba na hilo, serikali inapaswa kufata haki za walipa kodi, sera na sheria za kodi na utekelezaji wake uwe wa haki na wa wazi. Hivyo, hatuwezi kukwepa kulipa kodi maana watanzania ndio rasilimali kubwa ya serikali yetu inayoisadia kujipatia fedha kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom