w0rM
Member
- May 3, 2011
- 79
- 186
UTANGULIZI
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam almaarufu kama DIT ni moja ya vyuo vikongwe sana hapa nchini, chuo hiki kimetoa wataalamu mbalimbali kuanzia mafundi mchundo mpaka wahandisi katika kada mbalimbali. Ni ngumu kumkosa mtaalam kutoka DIT katika Taasisi yoyote ya Serikali na ya binafsi ndani ya Tanzania. Hii ni kutokana kwamba siku za nyuma elimu iliyotolewa katika taasisi hii ilikuwa ya vitendo zaidi. Kauli mbiu ya Serikali yetu ambayo pia imekuwa kauli ya nchi nzima ni kufikia Uchumi wa kati unaochochewa na Viwanda.
Ili kuwezesha maendeleo endelevu katika taifa letu ni lazima taasisi kama hii iwe na mchango mkubwa siyo tu katika kupika wataalamu wa Tanzania ya viwanda lakini pia kuibua bunifu zenye tija na zenye kuweza kutatua changamoto mbali mbali zinazolikabili taifa letu. Kwa sasa zipo changamoto nyingi zinazohafifisha uwezo wa Taasisi hii katika kuchangia maendeleo ya Taifa, changamoto hizi zimechambuliwa kwa kina na kutolewa maelezo na ushahidi wa kutosha lengo ikiwa ni kuifungua Serikali macho iweze kusimamia mabadiliko yanayohitajika na hatimaye Taasisi hii iweze kuleta mchango chanya kwa kizazi cha sasa na kwa vizazi vijavyo.
Hivi karibuni DIT imepata mkopo wa Bilioni 74 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuanzisha vituo viwili vya umahiri wa Tehama pamoja na uchakataji wa mazao ya ngozi. Hili ni deni kubwa sana kwa Taifa letu na kwa walipakodi wa Tanzania. Endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kubadili hali ya mambo, pesa hizi zitapotea na hazitaleta tija stahiki kwa Taifa.
Ripoti hii inaanza kwa kuainisha matatizo mbali mbali sugu yaliyopo DIT kwa ushahidi. Baada ya kuonyesha changamoto zilizopo pia inatoa historia ya matatizo sugu ya DIT, namna ambavyo uongozi wa sasa umeendelea kuchangia katika hayo matatizo, na inaainisha kuhusu uhitaji na umuhimu wa kuchukuliwa hatua za dhati kuinusuru DIT, na mwisho kabisa inatoa mapendekezo ya hatua stahiki zinazopaswa kuchukuliwa katika hatua ya awali ili kuinusuru DIT.
i. Ucheleweshwaji wa vifaa vya kufundishia (Teaching materials)
Kwa Taasisi kama DIT, suala la vifaa vya kufundishia ni suala la msingi na la kipaumbele pengine kushinda suala lolote lile. Hapa DIT suala la vifaa vya kufundishia limeendelea kuwa tatizo kwa muda mrefu na bajeti inayotengwa kwa ajili ya suala hili kilamwaka haiendani na uhalisia. Mfano, kitendo cha Taasisi kukosa vifaa vya kufundishia kwa muhula ulioanza 1/6/2020 mpaka 14/9/2020 siyo kitendo kizuri, waalimu wamelazimika kufundisha katika mazingira magumu sana vitu kama chaki, karatasi na marker pen hazikupatikana, hata kalamu za kusahihishia wafanyakazi wamelazimika kutafuta mabaki ya siku za nyuma na wengine kujinunulia kwa pesa zao mifukoni. Kwa upande wa vifaa vya maabara katika muhula huu vimechelewa sana kufika na vifaa vilivyostahili kuanza kutumika wakati wa mazoezi kwa vitendo vimeletwa mwishoni kabisa mwa muhula wakati wanafunzi wanakaribia kuanza mitihani hali iliyopelekea wanafunzi kukosa mazoezi ya vitendo ya kutosha.
iii. Ukosefu wa mtandao kwa waalimu
Tatizo la mtandao DIT siyo tu kwa wanafunzi, pia kwa waalimu wa DIT suala la mtandao limekuwa kama anasa kwa walimu, mtandao umekuwa wa kusuasua mara kadhaa na wakati mwingine waalimu wamekaa bila mtandao hata kwa wiki mbili kutokana na shida ndogo ndogo kama za AC kwenye vyumba vya kuhifadhia mitambo ya mtandao (server room). Pia kumekuwa na matatizo endelevu mfano katika jengo la mnara wa ufundishaji (teaching tower) hakuna mfumo wa kompyuta katika jengo lote, hii inamaanisha hakuna mtandao jengo zima. Inashangaza kwamba iliwezekanaje jengo kubwa kama hilo kujengwa DIT bila kuwekewa mifumo ya mawasiliano na yawezekana Serikali inayajua haya yote. Maswali yakiulizwa kuhusu maswala hayo majibu yake ni 'Mradi mkubwa wa Benki ya Dunia', eti mradi huo ndio utakuwa suluhisho la matatizo yote ya DIT. Wahadhiri na waalimu wanalazimika kutumia fedha zao za mifukoni ili kuwezesha upatikananji wa mtandao kwa ajili ya shughuli za taasisi, huku uongozi ukiwa kimya.
Katika jengo jipya la mnara wa ufundishaji (teaching tower) yapo madarasa hayana samani wala ubao jengo hilo lilizinduliwa rasmi mnamo 18/4/2018, lakini hadi leo tarehe 24/9/2020 hakuna kilichofanyika kubadili hali hiyo. Baadhi ya madarasa yasiyokuwa na samani angalia Picha 2 chini. Masuala ya kutafakari ni kuwa garama za kuweka samani katika baadhi ya vyumba inagharimu fedha kubwa kiasi gani na gharama kiasi gani zinahitajika kufanya marekebisho ya madarasa ya zamani ili kufanya mazingira ya usomaji yawe rafiki kwa wanafunzi wetu. Hapa ikumbukwe kuwa DIT ni taasisi inayopika na inayotoa mafundi na wahandisi katika maeneo yote hayo yenye changamoto.
v. Uchakavu na upungufu wa mashine na vifaa vya maabara vya kuwezesha mazoezi ya vitendo
Maabara za kufanyia mazoezi kwa vitendo DIT zimechoka kupita maelezo, vifaa vingi katika maabara hizo ni vifaa vya kizamani sana vifaa vipya ni kama havipo. Tukichukulia idara ya mitambo (Mechanical Engineering) kama mfano, mashine nyingi sana katika idara hiyo ni za kizamani sana, pamoja na uchakavu wa vifaa hivyo pia ripea za mara kwa mara ambazo ni muhimu ili kurefusha muda wa mashine kutumika imekosekana kwa muda mrefu sana. Mfano ukitembelea maabara ya uchomeleaji vyuma (welding), maabara ya mashine (machine shop), maabara ya magari (automobile workshop), maabara ya majokofu (refregeration ), maabara ya nishati (power plant), na maabara ya kufua chuma (foundry) katika idara ya ufundimitambo, utagundua kuwa hizi maabara zote ziko katika hali mbaya sana mashine nyingi zimepitwa na wakati na mashine nyingi zimekufa, au ziko karibu kufa. Baadhi ya mitambo iliyochoka angalia Picha 3 chini.
Idara ya mitambo ni moja ya idara ambazo wakati DIT inaanzishwa zilikuwa zinaibeba DIT hasa kutokana na mchango mkubwa katika jamii, lakini kwa sasa karibia inakufa kutokana na uchakavu wa maabara na upungufu mkubwa wa rasilimali watu wenye weledi na wabobezi. Kimsingi maabara hizi zimekuwa kama madampo ya vyuma chakavu. Wahusika wamejaribu kuelezea ukweli huu kwa viongozi wakuu wa taasisi lakini hakuna hatua zimechukuliwa ili kubadili hali hii.
Uongozi unawaagiza waalimu kutunga, kusahihisha na kupandisha matokeo ya wanafunzi huku wakijua uhalisia kuwa waalimu hawana vitendea kazi. Nalo hili suluhisho lake ni mradi wa benki ya dunia, yaani kwa sasa kila kitu DIT kinasubiri mradi wa benki ya dunia. Hapa pia tunaona ukosefu wa Vipaumbele.
Kwa upande wa wanafunzi hali ya mambo ni mbaya zaidi. Maabara karibia zote za kompyuta DIT zimekufa, tukianza na maabara ya Idara ya Mawasiliano ya anga ambayo ilikuwa imejaa kompyuta kipindi cha nyuma, hizo kompyuta zote zimekufa na hadi sasa hakuna hata kompyuta moja kwa ajili ya wanafunzi kutumia kufanyia mazoezi, ama za kutumika wakati wa kufundishia hasa kwa yale masomo yanayohitaji kompyuta. Vivyo hivyo maabara ya kompyuta iliyokuwa Idara ya Umeme, Idara ya Ujenzi, Idara ya Kompyuta pamoja na maeneo mengine ya Taasisi nyingi zimekufa. Baadhi ya maabara hizo zimeonyeshwa katika Picha 4,5,6 chini.
Sote tunafahamu uhalisia kuwa familia nyingi za kitanzania ambazo wanafunzi wengi wa DIT wanatoka ni masikini na hazina uwezo wa kuwanunulia watoto wao kompyuta, hivyo ufanisi wa wanafunzi kusoma teknolojia hasa kwa vitendo ni hafifu.
Nitoe mfano mdogo tu wa namna ambavyo mazingira yanaweza kuharibu ubora wa elimu hasa katika kipengele cha mitihani ambacho ndicho uongozi uliopo wa DIT unatilia maanani kama kigezo pekee cha ubora. Muhula wa kwanza 2019/2020 kabla ya janga la Korona wanafunzi wetu walifanya majaribio endelevu (continuous assessment) pamoja na baadhi ya mitihani ya mwisho katika bwalo kubwa la chakula, wakati huo feni katika bwalo hilo zilikuwa zimeharibika. Kutokana na ubovu wa feni hizo wanafunzi walilazimika kutoka nje mara kwa mara wengine hata kujimwagia maji vichwani ili kurudisha bongo zao katika utulivu kabla ya kuendelea na mitihani. Kwa upande wa wasimamizi walijikuta wanakaa karibu tu na milango au madirisha ili walau kupata hewa safi kutoka nje. Maana yake ni kwamba wasimamizi walikuwa hawasimamii kama ilivyostahili lakini haikuwa kutokana na utashi wao bali mazingira yaliwalazimisha.
Feni hizo zilikaa katika ubovu huo kwa kipindi cha zaidi ya mwaka bila kufanyiwa matengenezo stahiki, ikumbukwe kuwa DIT ni taasisi ya teknolojia ambayo inatoa wataalamu wa umeme kwenda kutataua matatizo ya jamii maeneo mbalimbali Tanzania, hivyo inashangaza kuona taasisi inashindwa kutataua matataizo yake madogo kama swala la feni kwa zaidi ya mwaka mzima.
Bajeti inayotengwa kwa ajili ya kazi za utafiti ni karibia na hakuna, na ikitoke kikatengwa hata kiasi ch asilimia 1 hakitolewi kwa ajili ya shughuli hizo, hivyo ni dhahiri kuwa hakuna dhamira ya kweli ya kuwezesha utafiti. Pia kutokana na uchache wa wafanyakazi DIT mhadhiri anajikuta anafanya kazi hata za msaidizi wa maabara wakatimwingine na kazi za msaidizi wa mhadhiri pia anafanya yeye hivyo kunakosekana muda wa kutosha wa wahadhiri kujihusisha na utafiti.
Kwa upande wa ushauri wa kiufundi kumekuwa na changamoto nyingi sana. Changamoto kubwa kuliko zote ni mtazamo hasi wa mkuu wa taasisi juu ya ushauri wa kiufundi (consultancy) mkuu aliyepo DIT kwa sasa anabeza majukumu ya ushauri wa kiufundi anasema kazi za ushauri wa kiufundi ni pesa nyepesi (cheap money) anasahau kuwa taasisi kubwa sana ya utaalamu wa kiufundi kwa vitendo katika Tanzania ni DIT na ina utofauti ukilinganisha na chuo kikuu cha dar es salaam ambacho ni mrengo wa nadharia zaidi. Hivyo DIT ipo katika nafasi nzuri sana ya kutoa ushauri wa kiufundi unaotokana na uzoefu wa kazi za vitendo na hilo ni jukumu tanzu kabisa la DIT. Hivyo mazingira ya wahadhiri wa DIT kushiriki katika kazi za ushauri wa kiufundi yameendelea kuwa magumu, hili linazorotesha hata uwezo wa wahadhiri kutoa elimu yenye ubora kwa weledi, maana sote tunafahamu kuwa ili kuwa na elimu bora ya vitendo ni lazima mhadhiri awe na mahusiano mazuri na endelevu na viwanda, hii itamuwezesha kujua teknolojia mpya na kuweza kujua mambo gani yamebadilika na namna tofauti ya kufanya vitu kwa umahiri. Kimsingi ukimchukua mhadhiri ambaye anahusika kufanya kazi za mtaani ukamlinganisha na yule ambaye anaishia kufundisha chuoni pekee, utakuta kuna tofauti kubwa sana hasa kwenye ubora wa elimu ambayo wanaitoa na hiyo iko wazi hata kwa wanafunzi. Walau kipindi hiki kuna baadhi ya wahadhiri wameenda viwandani kwa ajili ya mazoezi kwa vitendo (Industrial attachment) lakini ni kutokana na mradi wa Benki ya Dunia.
Tatizo lingine kubwa katika idara ya rasilimali watu ni ucheleweshwaji wa kupandisha watu madaraja hasa wafanyakazi wanapotoka masomoni. Kwa DIT kuna changamoto kubwa sana inayokatisha tamaa wafanyakazi, zipo hatua kadhaa za ndani ya DIT ambazo maranyingi huchelewesha mchakato wa kumpandisha daraja mtumishi. Mtumishi anpotoka shule anaweza akakaa hata Zaidi ya mwaka bila kupata barua ya uthibitisho wa ndani ya taasisi hata kama tayari ametimiza vigezo vyote vya uthibitisho kutoka TCU, tangu uongozi wa sasa wa DIT uingie madarakani tatizo hili limekuwa sugu sana na hii imepelekea watumishi wengi kukata tamaa kabisa.
Kuna wakati mtumishi anakuwa amepewa majukumu yanayoendana na cheo kipya ilhali hata barua ya ndani ya taasisi hajapatiwa ya kuthibitisha cheo hicho. Yaani kwa DIT watumishi wanateseka sana baada ya kutoka masomoni kana kwamba hawana haki katika taifa lao. Ikumbukwe kuwa wafanyakazi wa DIT wanapokwenda masomoni wanakutana na wenzao wanaotoka katika taasisi nyingine za Elimu ya Juu na taasisi nyingine za Serikali, cha ajabu ni kuwa wanaporudi wote kwa vipindi karibia vinavyofanana wale wafanyakazi wa taasisi nyingine kama UDSM, MUST na maeneo mengine wanakuwa wameshapata stahiki zao na hata mishahara yao inakuwa imeshapanda lakini kwa watumishi wa DIT inakuja kuchukua takriban miaka miwili na zaidi kwa hilo kutokea.
Mfano, mmoja kati ya watumishi alikabidhi vyeti baada ya kutoka masomoni na kuthibitishwa na TCU Disemba 2018 lakini mpaka sasa takriban mwaka na miezi minane hajapandishwa mshahara, yote ni kutokana na uzembe wa wahusika wa DIT maana hata barua ya ndani ya taasisi ya kumkubali kuwa Mhadhiri ameipata mwaka huu mwezi wa nne. Cha kustaajabisha zaidi ni kuwa wapo wafanyakazi kutoka taasisi nyingine ambao wamerudi mwaka jana katikati na wengine mwishoni lakini tayari kumekuwa na mabadiliko kwenye mishahara yao. Uzembe wa ndani ya taasisi unasababisha serikali ilaumiwe kwa kutopandisha madaraja na hivyo inabebeshwa mzigo isiyostahili.
Viongozi wa idara ya rasilimali watu wamekuwa wakilalamika kuwa Mkuu wa Taasisi hatoi ruhusa na wala haidhinishi fedha za kuiwezesha Idara kufuatilia masuala ya wafanyakazi kwa ukaribu Dodoma. Idara ikitaka kufanya ufuatiliaji na linapokuja suala la pesa mkuu wa taasisi anasema ataenda kushughulikia masuala ya wafanyakazi yeye mwenyewe akiwa Dodoma lakini mara zote hafuatilii wala kuyashughulikia akiwa Dodoma. Kimsingi ni kama anataka maisha ya watu wote DIT yawe magumu ili aendelee kuabudiwa maana yeye amejiweka kama Mungu wa DIT.
INAENDELEA...
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam almaarufu kama DIT ni moja ya vyuo vikongwe sana hapa nchini, chuo hiki kimetoa wataalamu mbalimbali kuanzia mafundi mchundo mpaka wahandisi katika kada mbalimbali. Ni ngumu kumkosa mtaalam kutoka DIT katika Taasisi yoyote ya Serikali na ya binafsi ndani ya Tanzania. Hii ni kutokana kwamba siku za nyuma elimu iliyotolewa katika taasisi hii ilikuwa ya vitendo zaidi. Kauli mbiu ya Serikali yetu ambayo pia imekuwa kauli ya nchi nzima ni kufikia Uchumi wa kati unaochochewa na Viwanda.
Ili kuwezesha maendeleo endelevu katika taifa letu ni lazima taasisi kama hii iwe na mchango mkubwa siyo tu katika kupika wataalamu wa Tanzania ya viwanda lakini pia kuibua bunifu zenye tija na zenye kuweza kutatua changamoto mbali mbali zinazolikabili taifa letu. Kwa sasa zipo changamoto nyingi zinazohafifisha uwezo wa Taasisi hii katika kuchangia maendeleo ya Taifa, changamoto hizi zimechambuliwa kwa kina na kutolewa maelezo na ushahidi wa kutosha lengo ikiwa ni kuifungua Serikali macho iweze kusimamia mabadiliko yanayohitajika na hatimaye Taasisi hii iweze kuleta mchango chanya kwa kizazi cha sasa na kwa vizazi vijavyo.
Hivi karibuni DIT imepata mkopo wa Bilioni 74 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuanzisha vituo viwili vya umahiri wa Tehama pamoja na uchakataji wa mazao ya ngozi. Hili ni deni kubwa sana kwa Taifa letu na kwa walipakodi wa Tanzania. Endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kubadili hali ya mambo, pesa hizi zitapotea na hazitaleta tija stahiki kwa Taifa.
Ripoti hii inaanza kwa kuainisha matatizo mbali mbali sugu yaliyopo DIT kwa ushahidi. Baada ya kuonyesha changamoto zilizopo pia inatoa historia ya matatizo sugu ya DIT, namna ambavyo uongozi wa sasa umeendelea kuchangia katika hayo matatizo, na inaainisha kuhusu uhitaji na umuhimu wa kuchukuliwa hatua za dhati kuinusuru DIT, na mwisho kabisa inatoa mapendekezo ya hatua stahiki zinazopaswa kuchukuliwa katika hatua ya awali ili kuinusuru DIT.
Changamoto za DIT
DIT inakabiliwa na changamoto kadhaa zinazohafifisha ubora na zinazoathiri upatikanaji wa elimu inayojikita zaidi katika vitendo (competence based). Hatuwezi kuzungumzia Tanzania ya viwanda bila kutilia maanani na mkazo elimu ya vitendo na elimu yenye kutatua changamoto za jamii yetu. Kwa muda mrefu huko nyuma DIT imekuwa ndiyo kiinua mgongo au alama ya elimu ya ufundi kwa vitendo katika taifa letu, alama hii kwa sasa iko taabani na inafifia kutokana na changamoto kadhaa. Baadhi ya changamoto sugu zinazoikabili DIT zimeainishwa hapa chini:i. Ucheleweshwaji wa vifaa vya kufundishia (Teaching materials)
Kwa Taasisi kama DIT, suala la vifaa vya kufundishia ni suala la msingi na la kipaumbele pengine kushinda suala lolote lile. Hapa DIT suala la vifaa vya kufundishia limeendelea kuwa tatizo kwa muda mrefu na bajeti inayotengwa kwa ajili ya suala hili kilamwaka haiendani na uhalisia. Mfano, kitendo cha Taasisi kukosa vifaa vya kufundishia kwa muhula ulioanza 1/6/2020 mpaka 14/9/2020 siyo kitendo kizuri, waalimu wamelazimika kufundisha katika mazingira magumu sana vitu kama chaki, karatasi na marker pen hazikupatikana, hata kalamu za kusahihishia wafanyakazi wamelazimika kutafuta mabaki ya siku za nyuma na wengine kujinunulia kwa pesa zao mifukoni. Kwa upande wa vifaa vya maabara katika muhula huu vimechelewa sana kufika na vifaa vilivyostahili kuanza kutumika wakati wa mazoezi kwa vitendo vimeletwa mwishoni kabisa mwa muhula wakati wanafunzi wanakaribia kuanza mitihani hali iliyopelekea wanafunzi kukosa mazoezi ya vitendo ya kutosha.
ii. Ukosefu wa mtandao (Internet) kwa wanafunzi
Katika karne ya 21 inastaajabisha kwa taasisi tena ya teknolojia kukosa kuwapatia wanafunzi wake huduma ya mtandao, teknolojia kwa sasa inapiga hatua kwa kasi sana, hivyo ili wanafunzi wetu waendane na kasi hiyo ni lazima wapate nafasi na uwezo wa kuangalia yanayoendelea duniani. Rais Magufuli wakati wa Uzinduzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma alisikika akisisitiza DIT itakuwa Kitovu cha tehama Tanzania; hili linahitaji taasisi hii kuwa connected vema. Wakati mwingine elimu inyotolewa kwenye mitandao ina ubora kuzidi vitini wanavyotoa walimu wetu ambavyo wakati mwingine vimepitwa na wakati na haviendani na uhalisia wala mahitaji ya soko la ajira. Kitendo cha wanafunzi wa DIT kukosa Mtandao si kizuri, wataalamu wanaoandaliwa lazima wawe na uwezo wa kulinganisha na kujifunza yanayofanywa na wenzao duniani. Kinyume cha hapo itakuwa teknolojia ya makaratasi ambayo haitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kutatua changamoto za kwenye jamii.iii. Ukosefu wa mtandao kwa waalimu
Tatizo la mtandao DIT siyo tu kwa wanafunzi, pia kwa waalimu wa DIT suala la mtandao limekuwa kama anasa kwa walimu, mtandao umekuwa wa kusuasua mara kadhaa na wakati mwingine waalimu wamekaa bila mtandao hata kwa wiki mbili kutokana na shida ndogo ndogo kama za AC kwenye vyumba vya kuhifadhia mitambo ya mtandao (server room). Pia kumekuwa na matatizo endelevu mfano katika jengo la mnara wa ufundishaji (teaching tower) hakuna mfumo wa kompyuta katika jengo lote, hii inamaanisha hakuna mtandao jengo zima. Inashangaza kwamba iliwezekanaje jengo kubwa kama hilo kujengwa DIT bila kuwekewa mifumo ya mawasiliano na yawezekana Serikali inayajua haya yote. Maswali yakiulizwa kuhusu maswala hayo majibu yake ni 'Mradi mkubwa wa Benki ya Dunia', eti mradi huo ndio utakuwa suluhisho la matatizo yote ya DIT. Wahadhiri na waalimu wanalazimika kutumia fedha zao za mifukoni ili kuwezesha upatikananji wa mtandao kwa ajili ya shughuli za taasisi, huku uongozi ukiwa kimya.
iv. Ubovu na uchache wa madarasa ya kufundishia
Madarasa mengi ya DIT ni mabovu sana yaani hakuna maintenance, yamechakaa utadhani hayapo katika taasisi ya teknolojia, unaweza ukafikiri ni magofu yaliyositishwa kutumika miaka kadhaa iliyopita, awali vijana wengi wa kitanzania wanajisikia ufahari wanapochaguliwa kujiunga na DIT lakini wanapofika mazingira yanawakatisha tamaa na kuwafanya wajione hawawezi kufanya kitu kizuri wala kikubwa. Wanashindwa kuelewa umuhimu wa kusoma uhandisi ambao hauwezi kutumika kutatua changamoto zinazowakabili katika mazingira yao ya DIT. Hii ni moja ya sababu inayopelekea wanafunzi wengi kusoma kwa ajili ya maksi tu na wanashindwa kuthubutu kufanya vitu vikubwa maana hawana imani kama inawezekana kufanya vitu vikubwa.Katika jengo jipya la mnara wa ufundishaji (teaching tower) yapo madarasa hayana samani wala ubao jengo hilo lilizinduliwa rasmi mnamo 18/4/2018, lakini hadi leo tarehe 24/9/2020 hakuna kilichofanyika kubadili hali hiyo. Baadhi ya madarasa yasiyokuwa na samani angalia Picha 2 chini. Masuala ya kutafakari ni kuwa garama za kuweka samani katika baadhi ya vyumba inagharimu fedha kubwa kiasi gani na gharama kiasi gani zinahitajika kufanya marekebisho ya madarasa ya zamani ili kufanya mazingira ya usomaji yawe rafiki kwa wanafunzi wetu. Hapa ikumbukwe kuwa DIT ni taasisi inayopika na inayotoa mafundi na wahandisi katika maeneo yote hayo yenye changamoto.
v. Uchakavu na upungufu wa mashine na vifaa vya maabara vya kuwezesha mazoezi ya vitendo
Maabara za kufanyia mazoezi kwa vitendo DIT zimechoka kupita maelezo, vifaa vingi katika maabara hizo ni vifaa vya kizamani sana vifaa vipya ni kama havipo. Tukichukulia idara ya mitambo (Mechanical Engineering) kama mfano, mashine nyingi sana katika idara hiyo ni za kizamani sana, pamoja na uchakavu wa vifaa hivyo pia ripea za mara kwa mara ambazo ni muhimu ili kurefusha muda wa mashine kutumika imekosekana kwa muda mrefu sana. Mfano ukitembelea maabara ya uchomeleaji vyuma (welding), maabara ya mashine (machine shop), maabara ya magari (automobile workshop), maabara ya majokofu (refregeration ), maabara ya nishati (power plant), na maabara ya kufua chuma (foundry) katika idara ya ufundimitambo, utagundua kuwa hizi maabara zote ziko katika hali mbaya sana mashine nyingi zimepitwa na wakati na mashine nyingi zimekufa, au ziko karibu kufa. Baadhi ya mitambo iliyochoka angalia Picha 3 chini.
Idara ya mitambo ni moja ya idara ambazo wakati DIT inaanzishwa zilikuwa zinaibeba DIT hasa kutokana na mchango mkubwa katika jamii, lakini kwa sasa karibia inakufa kutokana na uchakavu wa maabara na upungufu mkubwa wa rasilimali watu wenye weledi na wabobezi. Kimsingi maabara hizi zimekuwa kama madampo ya vyuma chakavu. Wahusika wamejaribu kuelezea ukweli huu kwa viongozi wakuu wa taasisi lakini hakuna hatua zimechukuliwa ili kubadili hali hii.
vi. Ukosefu wa vitendea kazi kama kompyuta kwa wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Taasisi
Moja kati ya changamoto kubwa sana kwa wafanyakazi wa DIT hasa walioajiriwa ndani ya miaka kama sita iliyopita ni ukosefu wa vitendea kazi. Moja ya kitendea kazi kikubwa sana kwa mwalimu hasa kwa karne hii ni kompyuta ambayo humuwezesha mwalimu kuandaa mada za kufundisha, kuandaa mitihani, pamoja na kupandishia matokeo kwenye mtandao baada ya kusahihisha. Kuna wafanyakazi ambao wamekaa DIT kwa takriban miaka sita sasa bila kuwa na kompyuta, uongozi wa juu wa taasisi unafahamu uhalisia wa jambo hili lakini hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kutatua changamoto za waalimu.Uongozi unawaagiza waalimu kutunga, kusahihisha na kupandisha matokeo ya wanafunzi huku wakijua uhalisia kuwa waalimu hawana vitendea kazi. Nalo hili suluhisho lake ni mradi wa benki ya dunia, yaani kwa sasa kila kitu DIT kinasubiri mradi wa benki ya dunia. Hapa pia tunaona ukosefu wa Vipaumbele.
Kwa upande wa wanafunzi hali ya mambo ni mbaya zaidi. Maabara karibia zote za kompyuta DIT zimekufa, tukianza na maabara ya Idara ya Mawasiliano ya anga ambayo ilikuwa imejaa kompyuta kipindi cha nyuma, hizo kompyuta zote zimekufa na hadi sasa hakuna hata kompyuta moja kwa ajili ya wanafunzi kutumia kufanyia mazoezi, ama za kutumika wakati wa kufundishia hasa kwa yale masomo yanayohitaji kompyuta. Vivyo hivyo maabara ya kompyuta iliyokuwa Idara ya Umeme, Idara ya Ujenzi, Idara ya Kompyuta pamoja na maeneo mengine ya Taasisi nyingi zimekufa. Baadhi ya maabara hizo zimeonyeshwa katika Picha 4,5,6 chini.
Sote tunafahamu uhalisia kuwa familia nyingi za kitanzania ambazo wanafunzi wengi wa DIT wanatoka ni masikini na hazina uwezo wa kuwanunulia watoto wao kompyuta, hivyo ufanisi wa wanafunzi kusoma teknolojia hasa kwa vitendo ni hafifu.
vii. Ubovu, uchakavu, na ufinyu wa nafasi katika ofisi ya mitihani
Moja ya vitu vya msingi sana katika Taasisi yoyote ya elimu ni mitihani maana ndiyo njia ya moja kwa moja ambayo imetumika kupima uwezo wa wanafunzi kwa miaka mingi, hivyo kwa taasisi ambayo ina viongozi makini na wanaotoa kipaumbele katika ubora wa elimu lazima ofisi ya mitihani iwe na ubora unaostahili. Hapa DIT mambo ni tofauti, ofisi ndogo ambayo ilitumika tangu enzi za DTC wakati wanafunzi walipokuwa wachache ndiyo inayotumika mpaka sasa, ofisi ni finyu sana na imechakaa sana haina hadhi hata ya kuitwa ofisi ya mitihani, ukiingia unaweza kudhani ni stoo. Hapa karibuni takriban mwezi kabla ya mitihani ya muhula wa pili 2019/2020 kuanza, mvua iliharibu baadhi ya nyaraka maana paa lilichakaa mpaka likawa linapitisha maji na kupelekea kuloa kwa baadhi ya nyaraka hizo. Baada ya nyaraka kuloa ndipo ofisi ya mitihani imefanyiwa marekebisho ya paa. Hii inaonyesha moja kwa moja ukosefu wa vipaumbele katika taasisi. Masuala ya msingi kama hayo hayashughulikiwi mpaka madhara yatokee. Mpaka tunavyoongea tofauti na suala la paa bado ofisi imechakaa sana na ni finyu, ni aibu hata kukiita kile chumba ofisi ya mitihani ya DIT, taasisi inayoandaa wataalamu kwa ajili ya kutumika nchini lakini inashindwa kuwatumia wataalamu wake hao hao kutatua changamoto zake yenyewe.viii. Changamoto katika kusimamia uthibiti wa ubora wa elimu(Quality assurance and Quality control)
Ubora wa elimu limeendelea kuzorota sana DIT, uongozi unadhani kuwa ubora wa elimu unaangaliwa tu wakati wa usimamizi wa mitihani. Hii ndiyo maana vifaa vya kufundishia vinaweza kuchelewa na hakuna anayejali. Sote tunafahamu kuwa ubora unachangiwa na mambo mengi mojawapo ikiwa ni suala la mazingira elimu inapotolewa, suala zima la ufundishaji hasa uwepo wa elimu kwa vitendo na mwisho ndipo suala la mitihani linafuata. Changamoto za DIT zinavuruga ubora kwa kuwa maeneo yote matatu ya msingi yaliyotajwa yana shida.Nitoe mfano mdogo tu wa namna ambavyo mazingira yanaweza kuharibu ubora wa elimu hasa katika kipengele cha mitihani ambacho ndicho uongozi uliopo wa DIT unatilia maanani kama kigezo pekee cha ubora. Muhula wa kwanza 2019/2020 kabla ya janga la Korona wanafunzi wetu walifanya majaribio endelevu (continuous assessment) pamoja na baadhi ya mitihani ya mwisho katika bwalo kubwa la chakula, wakati huo feni katika bwalo hilo zilikuwa zimeharibika. Kutokana na ubovu wa feni hizo wanafunzi walilazimika kutoka nje mara kwa mara wengine hata kujimwagia maji vichwani ili kurudisha bongo zao katika utulivu kabla ya kuendelea na mitihani. Kwa upande wa wasimamizi walijikuta wanakaa karibu tu na milango au madirisha ili walau kupata hewa safi kutoka nje. Maana yake ni kwamba wasimamizi walikuwa hawasimamii kama ilivyostahili lakini haikuwa kutokana na utashi wao bali mazingira yaliwalazimisha.
Feni hizo zilikaa katika ubovu huo kwa kipindi cha zaidi ya mwaka bila kufanyiwa matengenezo stahiki, ikumbukwe kuwa DIT ni taasisi ya teknolojia ambayo inatoa wataalamu wa umeme kwenda kutataua matatizo ya jamii maeneo mbalimbali Tanzania, hivyo inashangaza kuona taasisi inashindwa kutataua matataizo yake madogo kama swala la feni kwa zaidi ya mwaka mzima.
ix. Kudorora kwa maswala ya utafiti na ushauri wa kiufundi
Moja ya majukumu muhimu sana kwa wahadhiri wa taasisi za elimu ya juu katika taifa letu ni kushiriki kufanya tafiti zenye tija na zenye kuleta suluhisho la matatizo mbali mbali tuliyonayo katika jamii. Ili haya yawezekane ni lazima mazingira ya kufanyia kazi yawe rafiki kuwezesha utafiti kufanyika, ni dhahiri kwamba kama mhadhiri mwenye (PhD) anakosa japo compyuta ya kufanyia kazi za kawaida ofisini basi siyo rahisi akapata uwezeshaji mwingine unaostahili ili aweze kufanya utafiti wenye tija na manufaa kwa taifa. Kwa namna nyingine ni dhahiri kwamba kama mazingira ya kawaida tu ya kufundishia na uwezeshaji wa kawaida tu ili kumuwezesha mwalimu kufundisha kwa weledi haiwezekani, basi ni ndoto kwa utafiti wenye tija kufanyika.Bajeti inayotengwa kwa ajili ya kazi za utafiti ni karibia na hakuna, na ikitoke kikatengwa hata kiasi ch asilimia 1 hakitolewi kwa ajili ya shughuli hizo, hivyo ni dhahiri kuwa hakuna dhamira ya kweli ya kuwezesha utafiti. Pia kutokana na uchache wa wafanyakazi DIT mhadhiri anajikuta anafanya kazi hata za msaidizi wa maabara wakatimwingine na kazi za msaidizi wa mhadhiri pia anafanya yeye hivyo kunakosekana muda wa kutosha wa wahadhiri kujihusisha na utafiti.
Kwa upande wa ushauri wa kiufundi kumekuwa na changamoto nyingi sana. Changamoto kubwa kuliko zote ni mtazamo hasi wa mkuu wa taasisi juu ya ushauri wa kiufundi (consultancy) mkuu aliyepo DIT kwa sasa anabeza majukumu ya ushauri wa kiufundi anasema kazi za ushauri wa kiufundi ni pesa nyepesi (cheap money) anasahau kuwa taasisi kubwa sana ya utaalamu wa kiufundi kwa vitendo katika Tanzania ni DIT na ina utofauti ukilinganisha na chuo kikuu cha dar es salaam ambacho ni mrengo wa nadharia zaidi. Hivyo DIT ipo katika nafasi nzuri sana ya kutoa ushauri wa kiufundi unaotokana na uzoefu wa kazi za vitendo na hilo ni jukumu tanzu kabisa la DIT. Hivyo mazingira ya wahadhiri wa DIT kushiriki katika kazi za ushauri wa kiufundi yameendelea kuwa magumu, hili linazorotesha hata uwezo wa wahadhiri kutoa elimu yenye ubora kwa weledi, maana sote tunafahamu kuwa ili kuwa na elimu bora ya vitendo ni lazima mhadhiri awe na mahusiano mazuri na endelevu na viwanda, hii itamuwezesha kujua teknolojia mpya na kuweza kujua mambo gani yamebadilika na namna tofauti ya kufanya vitu kwa umahiri. Kimsingi ukimchukua mhadhiri ambaye anahusika kufanya kazi za mtaani ukamlinganisha na yule ambaye anaishia kufundisha chuoni pekee, utakuta kuna tofauti kubwa sana hasa kwenye ubora wa elimu ambayo wanaitoa na hiyo iko wazi hata kwa wanafunzi. Walau kipindi hiki kuna baadhi ya wahadhiri wameenda viwandani kwa ajili ya mazoezi kwa vitendo (Industrial attachment) lakini ni kutokana na mradi wa Benki ya Dunia.
x. Upungufu wa rasilimali watu (Human resource) na manyanyaso kwa wafanyakazi
Moja ya changamoto kubwa sana zinazoikabili DIT ni upungufu mkubwa wa rasilimali watu, Wakufunzi wengi sana wamestaafu bila kuwepo na mpango wa urithishwaji ujuzi mzuri, changamoto hii imekuwepo kwa muda mrefu sana katika idara nyeti za DIT kama Umeme, Mitambo, Ujenzi na idara zingine. Kwa upande mwingine wafanyakazi wengi sana wamehama DIT katika miaka ya hivi karibuni (2016-2020) kutokana na mazingira magumu ya kufanya kazi, kimsingi wafanyakazi wengine waliopo DIT wameomba kuhama lakini wamekataliwa na wizara kwa madai kwamba DIT haina wafanyakazi wa kutosha. Takriban wafanyakazi wanne kutoka katika ofisi ya idara ya rasilimali watu wamehama DIT, kimsingi idara hiyo ndiyo inapaswa kuleta chachu na kuwezesha wafanyakazi wengine watamani kuendelea kufanya kazi DIT lakini wao wenyewe hawana matumaini na wanahama. Unapoona wanaopaswa kuhamasisha wafanyakazi kuendelea kufanya kazi wanahama unagundua kuna tatizo kubwa sana DIT. Kwa sasa asilimia kubwa ya wafanyakazi wa DIT wangeulizwa kama wanatamani kuendelea kubaki au waondoke DIT zaidi ya asilimia tisini wangechagua kuondoka.Tatizo lingine kubwa katika idara ya rasilimali watu ni ucheleweshwaji wa kupandisha watu madaraja hasa wafanyakazi wanapotoka masomoni. Kwa DIT kuna changamoto kubwa sana inayokatisha tamaa wafanyakazi, zipo hatua kadhaa za ndani ya DIT ambazo maranyingi huchelewesha mchakato wa kumpandisha daraja mtumishi. Mtumishi anpotoka shule anaweza akakaa hata Zaidi ya mwaka bila kupata barua ya uthibitisho wa ndani ya taasisi hata kama tayari ametimiza vigezo vyote vya uthibitisho kutoka TCU, tangu uongozi wa sasa wa DIT uingie madarakani tatizo hili limekuwa sugu sana na hii imepelekea watumishi wengi kukata tamaa kabisa.