Changamoto ya mfumo wa kutuma maombi ya ajira kwa nafasi za kazi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA))

MubengaJr

Senior Member
Oct 14, 2022
141
323
Kwa muda takribani wiki sasa, nimekuwa nikijaribu kutuma maombi ya kazi kupitia mfumo wa ajira wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) bila mafanikio. Niwaombe Mamlaka watoke hadharani na kutoa tamko kuhusu changamoto hizi na mwelekeo (Way forward).

Kuna wakati napata hisia mbaya kwamba tayari wameandaa watu wao. Aidha kwa wale ambao mmefanikiwa kutuma maombi tunaomba mtushirikishe namna ambavyo mmeweza kufanikisha utumaji wa maombi.

Kwa upande wangu nimejaza taarifa zote lakini kila nikitaka kufanya maombi napata ujumbe uliopo kwenye kiambatisho hapa chini

Naomba kuwasilisha.

 
Ivyo vitu ujajaza vijaze ndio utume maombi system iko poa amka usiku saa nane tuma kila la kheri
 
system inakaa poa usiku kuanzia saa tatu, wala haisumbui ila mchana kimbembe
 
Ivyo vitu ujajaza vijaze ndio utume maombi system iko poa amka usiku saa nane tuma kila la kheri
inakuwaje avijaze wakati sio vya lazima ni optional hapo pa kujaza ni qualification tu lkn pia hii system inafanya watu kukosa nafasi ya kuapply maana its too much kwakweli huyu server wao wanaomtumia sijui ARUTI poor na kwanini kila kipengele ikijsza lzm iroad kwanini isisubir umalize kujaza unapoa add ndio iload yaan ni majanga kwakweli
 
Mkuu hopefully ulifanikiwa kutuma maombi. Ki kawaida kazi hizi watu wanakuwa ni wengi wanatuma maombi inapelekea system kuwa down.
Kama wewngine walivyotoa maoni yao muda mzuri wa kutuma maombi ni usiku tu kuanzia saa tatu huko mpaka saa 12 asubuhi.
Pia unaweza pitia uzi huu hapa chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…