Uchaguzi 2025 Chama Tawala na Vyama vya upinzani vimeshindwa kutuletea mabadiliko na ustawi. Wananchi tufanye nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

tripof

JF-Expert Member
Apr 2, 2024
761
1,039
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama tawala CCM na pia Vyama vya Upinzani, nimegundua hakuna chama kinachoweza kutuletea mabadiliko ya kweli. Matokeo yake akina Msigwa, Mwita Waitara, Prof Mkumbo, Mashinji, Gekul, Katambi nk kuhama na kutafuta maslahi binafsi zaidi.

Upande wa pili CCM inatafuta kila njia ya kutumia kodi za wananchi kwenye mambo yasiyo na maslahi ya wananchi zaidi ya kufuja raslimali za nchi na kujinufaisha wao wenyewe.

Je, tufanye nini sasa iwapo upinzani ni tatizo na Chama Tawala tatizo. Tukimblie wapi.Nisaidieni kupata suluhisho na mwafaka.
 
Siku tukijitambua tutajua chakufanya. Kwani unadhani watz hawaoni kinachoendelea Kenya? Siku tukitimiza wajibu wetu kama Wananchi kila kitu kitakwenda sawa.
 
KUNA USEMI WA ALIKIBA KIPINDI FLANI ALIMWAMBIA DIAMOND.. 'UNANIIBIA PENCIL ALAFU UNAJIDAI KUNISAIDIA KUITAFTA' exactly kinachotokea Kwa wanasiasa wa tanzania
 
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama tawala CCM na pia Vyama vya Upinzani, nimegundua hakuna chama kinachoweza kutuletea mabadiliko ya kweli. Matokeo yake akina Msigwa,Mwita Waitara,Prof Mkumbo, Mashinji, Gekul, Kitambi nk kuhama na kutafuta maslahi binafsi zaidi. Upande wa pili CCM inatafuta kila njia ya kutumia kodi za wananchi kwenye mambo yasiyo na maslahi ya wananchi zaidi ya kufuja raslimali za nchi na kujinufaisha wao wenyewe. je tufanye nini sasa iwapo upinzani ni tatizo na Chama Tawala tatizo. Tukimblie wapi.Nisaidieni kupata suluhisho na mwafaka.
Jibu ni katiba ya wananchi inayoendana na tabia uchawa hata unyumbu, (a.k.a kujizima data), bila kusahau utandawazi na mila zetu
 
..Ccm ruzuku bil 13 kwa mwezi.

..Cdm ruzuku mil 10 kwa mwezi.

..halafu tunadai huduma sawa toka vyama hivyo.
 
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama tawala CCM na pia Vyama vya Upinzani, nimegundua hakuna chama kinachoweza kutuletea mabadiliko ya kweli. Matokeo yake akina Msigwa,Mwita Waitara,Prof Mkumbo, Mashinji, Gekul, Kitambi nk kuhama na kutafuta maslahi binafsi zaidi. Upande wa pili CCM inatafuta kila njia ya kutumia kodi za wananchi kwenye mambo yasiyo na maslahi ya wananchi zaidi ya kufuja raslimali za nchi na kujinufaisha wao wenyewe. je tufanye nini sasa iwapo upinzani ni tatizo na Chama Tawala tatizo. Tukimblie wapi.Nisaidieni kupata suluhisho na mwafaka.
Cha msingi pigania familia yako, uchumi wako, acha kufuatilia mambo ya siasa, kwa mtazamo wangu:

-Wafanya kazi wapiganie maslahi yao kuliko kuwanyeyekea wanasiasa, mkiwakabidhi wanasiasa kupigania maslahi yenu watayafanyia siasa
- Wakulima wapambe na hali zao wasiwakabidhi wanasiasa
-Wafanya biashara na wao hivyo hivyo. Yaani asijitokeze mtu anasema nawapigania wanyonge, wanaishia kutunyonga, asijitokeze mtu anasema nawatumikia wananchi, kila mtu ajitumikie kivyake
 
Acha ukilaza ni lini upinzani uliongoza hili TAIFA?
 
Upinzania ni Ideology na sio Chama, rudi Darasani ukasome. Pia mageuzi hayaletwi na Chama yanaletwa na watu rai. sasa kaaa ukingojea Mbowe au Lisu akuletee mageuzi wewe ukiwa umekaa pembeni ya Tv, na huu ndio ujinga wa wabongo.
 
Cha msingi pigania familia yako, uchumi wako, acha kufuatilia mambo ya siasa, kwa mtazamo wangu:

-Wafanya kazi wapiganie maslahi yao kuliko kuwanyeyekea wanasiasa, mkiwakabidhi wanasiasa kupigania maslahi yenu watayafanyia siasa
- Wakulima wapambe na hali zao wasiwakabidhi wanasiasa
-Wafanya biashara na wao hivyo hivyo. Yaani asijitokeze mtu anasema nawapigania wanyonge, wanaishia kutunyonga, asijitokeze mtu anasema nawatumikia wananchi, kila mtu ajitumikie kivyake
Unapigania Familia ipi? Ujinga mwingi, nazani nyie ndio wale mkisha jenga nyumba na kuwa na uwezo wa kubadili milo mnaona mmemaliza maisha na hata nchi ikiuzwa hakuna shida make una nyumba na gari la mtumba kutoka Japani.

Vipi wakaja watawala na wakakumbia unapswa kubomoa hio nyumba yako na uhame hapo? Pale tarafa ya Ngorongoro kuna Wamasai walikuwa wamejenga majengo ya maana sana na walikuwa na mawazo kama yako, leo hii nyumba zimebomolewa na kule Handeni nyumba zote ni ramani moja kama nyumba za manamba.

Sasa wewe endele kujidanganya kwamba unapigania familia na mengine hayakuhusu, labda kama wewe na hio familia yako mnakaa Mars.

Ukiona watu hawana ajira unaona hayakuhusu kwa sababu wewe unayo, Ukiona wamama wamelala mzungu wa nne hosipitalini unaona hayakuhusu kwa saba wewe una Bima ya afya so wanao lala mzungu wa nne ni wajinga fulani kuna siku utavamiwa na hao wasio kuwa na ajira au wanaweza kukua kabisa na kuondoka hata na simu.Acha ujinga.
 
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama tawala CCM na pia Vyama vya Upinzani, nimegundua hakuna chama kinachoweza kutuletea mabadiliko ya kweli. Matokeo yake akina Msigwa,Mwita Waitara,Prof Mkumbo, Mashinji, Gekul, Kitambi nk kuhama na kutafuta maslahi binafsi zaidi. Upande wa pili CCM inatafuta kila njia ya kutumia kodi za wananchi kwenye mambo yasiyo na maslahi ya wananchi zaidi ya kufuja raslimali za nchi na kujinufaisha wao wenyewe. je tufanye nini sasa iwapo upinzani ni tatizo na Chama Tawala tatizo. Tukimblie wapi.Nisaidieni kupata suluhisho na mwafaka.
Upinzani hauwezii kufanya mabadiliko yeyote bila kuwa na nguvu kutoka kwa wananchi nyuma Yao, upinzani ambao ukitangaza maandamano wanaenda peke Yao unafikirii upinzani utapata vipi nguvuu,,wananchi wa Tz wengi hatujitambuii na simply ni kwa sababu wananchi wengi wa TZ hawana maisha mangumu (hawana njaa),,,
 
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama tawala CCM na pia Vyama vya Upinzani, nimegundua hakuna chama kinachoweza kutuletea mabadiliko ya kweli. Matokeo yake akina Msigwa,Mwita Waitara,Prof Mkumbo, Mashinji, Gekul, Kitambi nk kuhama na kutafuta maslahi binafsi zaidi. Upande wa pili CCM inatafuta kila njia ya kutumia kodi za wananchi kwenye mambo yasiyo na maslahi ya wananchi zaidi ya kufuja raslimali za nchi na kujinufaisha wao wenyewe. je tufanye nini sasa iwapo upinzani ni tatizo na Chama Tawala tatizo. Tukimblie wapi.Nisaidieni kupata suluhisho na mwafaka.
anzisha chama chako mwenyewe, chenye sera na mipango mbadala na bora zaido ya unao walaumu.,,:pulpTRAVOLTA:

mabadiliko yanaanza na wewe, lawama hazina msingi wala maana:pulpTRAVOLTA:
 
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataleta viongozi wanaotakiwa na wananchi, sio viongozi wanaoteuliwa na kigenge cha majizi yajiitayo system.
 
Unapigania Familia ipi? Ujinga mwingi, nazani nyie ndio wale mkisha jenga nyumba na kuwa na uwezo wa kubadili milo mnaona mmemaliza maisha na hata nchi ikiuzwa hakuna shida make una nyumba na gari la mtumba kutoka Japani.

Vipi wakaja watawala na wakakumbia unapswa kubomoa hio nyumba yako na uhame hapo? Pale tarafa ya Ngorongoro kuna Wamasai walikuwa wamejenga majengo ya maana sana na walikuwa na mawazo kama yako, leo hii nyumba zimebomolewa na kule Handeni nyumba zote ni ramani moja kama nyumba za manamba.

Sasa wewe endele kujidanganya kwamba unapigania familia na mengine hayakuhusu, labda kama wewe na hio familia yako mnakaa Mars.

Ukiona watu hawana ajira unaona hayakuhusu kwa sababu wewe unayo, Ukiona wamama wamelala mzungu wa nne hosipitalini unaona hayakuhusu kwa saba wewe una Bima ya afya so wanao lala mzungu wa nne ni wajinga fulani kuna siku utavamiwa na hao wasio kuwa na ajira au wanaweza kukua kabisa na kuondoka hata na simu.Acha ujinga.
Endelea kuwanyeyekea wanasiasa, wana siasa wakuletee ajira? haohao wanasiasa ndo wanakaa bungeni kusema kiswahili kitumike kufundisha shuleni wakati watoto wao wanasoma nje ya nchi, ndo unawategemea? achana na mawazo ya nchi kuuzwa umeshasikia nchi gani imeuzwa? kama Mungu amekupa ajira, fanya kwa bidii kwa ajili ya kizazi chako, hata usipokuwepo watajua uliwapigania, Hao hao wanasiasa wanakuambia jiajirini wakat wao wanapigania hizo ajira hata kwa kuroga. Amka usingizini

Hao wanasiasa hawana msimamo kila kukicha kila mtu anapigania tumbo lake. Yesu mwenye alisema "enyi wanawake wa Yerusalem jililieni ninyi na watoto wenu"
 
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataleta viongozi wanaotakiwa na wananchi, sio viongozi wanaoteuliwa na kigenge cha majizi yajiitayo system.
Hapana hayo Mapinduzi ya kijeshi yamefanyika kwenye nchi za wenzetu, je maisha yao yamekuwa bora? je wamepata viongozi walio bora?
 
Upinzania ni Ideology na sio Chama, rudi Darasani ukasome. Pia mageuzi hayaletwi na Chama yanaletwa na watu rai. sasa kaaa ukingojea Mbowe au Lisu akuletee mageuzi wewe ukiwa umekaa pembeni ya Tv, na huu ndio ujinga wa wabongo.
Na ndio ujinga mkubwa, et utegemee wanasiasa.

Kuna kijiji nimekipenda huko Rukwa, wao kwenye shughuli za kujenga madarasa kwa ajili ya watoto wao, kila mwanakijiji anachangia tofali 200, na fedha taslimu, yaani wameamua kujipambania wenyewe, ukingoja mwanasiasa atapika mboyoyo tu
 
Hapana hayo Mapinduzi ya kijeshi yamefanyika kwenye nchi za wenzetu, je maisha yao yamekuwa bora? je wamepata viongozi walio bora?
Bora kusiwe na hayo maisha mazuri, kuliko kuendelea kutawaliwa na ccm kwa shuruti.
 
Back
Top Bottom