Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) chataka Matumizi ya kitita cha NHIF yasitishwe, chashauri viwepo vitita tofauti kwa Serikali na Private

Heparin

JF-Expert Member
Sep 24, 2021
218
1,066
Pharmaceutical Society of Tanzania (PST) ni chama cha kitaaluma, kwa taaluma ya famasi nchini. Baadhi ya
malengo yake ni kuboresha na kukuza ubora wa huduma na shughuli za dawa, kuweka ushawishi sahihi na wenye maslahi/faida kwa watanzania katika masuala ya afya.

Tunashukuru Wizara ya Afya kuona umuhimu na kutushirikisha katika hatua hii ya maoni ya maboresho ya
kitita cha mfuko wa bima ya taifa ya afya (NHIF) na ni matumaini yetu maoni yetu yatachukuliwa kwa uzito
stahiki.

Baada ya kupitia ripoti ya NHIF ya 2022, PST imejiridhisha kwamba bei za huduma na bidhaa za afya haikua
miongoni mwa changamoto za mfuko, na hii inaondoa mantiki nzima ya maamuzi haya ya sasa ya
kupunguza bei hizo. Kadhalika taarifa ya Mkaguzi 2022 imeonesha changamoto za mfuko ambapo bei za bidhaa kama zilivyo katika kitita cha awali haikua miongoni mwa changamoto hizo.

PST inapendekeza Fedha za mfuko zilizo kama madeni zirejeshwe mapema iwezekanavyo, Fedha za mfuko zitumike tu kulipia gharama za shughuli za mfuko zenye tija kwa wanufaika, na kwa asilimia zilizopangwa, upanuzi wa huduma uende kwa kasi ya uchumi na kadiri kila mtoa huduma ataona uhitaji wa soko. Pia, hatua kali zichukuliwe kwa wote waliobainika kushiriki katika udanganyifu.

Aidha, PST imebaini mambo yafuatayo;
  • Dawa 57 (11%) kati ya zilizofanyiwa uchambuzi zina bei (NHIF) chini ya bei ya msambazaji kabla ya kuweka markup ya 40%, zinaongezeka na kuwa dawa 149 (29%) baada ya kuweka markup
  • Ukiweka katika makundi dawa hizo 57 kulinganisha na manunuzi ziko hasi (negative) kama ifuatavyo 19 (0 to -25%), 22 (-26% to -50%), 13 (-51% to -75%) na 3 (>-76%), hali hii inakua mbaya zaidi zinapowekwa markup ya 40% kama ilivyo katika jedwali
  • Tumetambua kuwa baadhi ya bei za bidhaa katika kitita zimefanyiwa rejea kwenye orodha ya dawa za Bohari ya Dawa (MSD)
Baada ya uchambuzi na ulinganifu huo hapo juu na kwa kuzingatia muda mchache tuliokua nao, PST
inapendekeza yafuatayo:
  • Matumizi ya kitita hiki yasitishwe na kiundwe chombo huru chenye wataalamu na weledi kitakachosimamia masuala ya gharama za matibabu tanzania (kipewe miezi sita)
  • Hata baada ya kupata kitita kipya, kuwe na muda wa mpito (grace period) kabla ya kuanza kutumika ili kuepusha hasara zinazowezajitokeza
  • Jukumu la hospitali iwe kuhudumia wagonjwa wa ndani (inpatients), polyclinics kutoweka dawa kwani kimuundo hazipaswi, hii itapunguza mgongano wa maslahi na matumizi yasiyosahihi ya dawa
  • Tuchukue na maamuzi magumu lakini sahihi , hasa tunapoelekea kwenye Universal Health Coverage, ya kuwapa uhuru na kuwaruhusu wagonjwa kuchukua vyeti vyao vya dawa na kuhudumiwa katika famasi za jamii (community pharmacy) ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa mikataba ya NHIF na famasi
  • NHIF waanze kuruhusu utaratibu wa kuchangia (co-payment/top up) endapo mtaalamu amejiridhisha huduma au dawa husika ina manufaa kwa mgonjwa na mgonjwa ameridhia, hii itaongeza treatment satisfaction and outcome
  • Kuwepo na Kitita tofauti cha vituo binafsi (Private) na Umma (Public) kwani huduma za binafsi zina gharama kubwa Zaidi ya uendeshaji kuliko vituo vya Umma mfano Majengo, malazi, gharama za watumishi.
 

Attachments

  • PST NHIF Kitita maoni- edited (1).pdf
    574.7 KB · Views: 6
Back
Top Bottom