Chama cha Ushirika-TANECU kitulipe malipo ya Korosho, mchakato unachelewa sana na kutuathiri Wakulima wa Mtwara

Nyakijooga

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
275
471
Mimi ni mkazi wa Mtwara, nina lalamiko kuhusiana na malipo ya korosho kupitia Chama cha Ushirika-TANECU (Tandahimba-Newala Cooperative Union) umefanyika mnada wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa nne.

Malipo yaliyofanyika ni ya mnada wa kwanza na mnada wa pili ambapo baadhi ya Wakulima ndio wamelipwa.

Nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara kupitia Makarani kwamba shida ni Nini? Wanadai wame-submit taarifa zote za malipo Payment Centers lakini bado inachukua muda mrefu kuchakatwa.
 
Back
Top Bottom