Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,724
- 4,475
Wakuu,
Chama cha National League for Democracy (NLD) kimesema kitaendelea kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 licha ya changamoto za kisiasa.
Akizungumza Februari 23, 2025, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa NLD, Doyo Hassan Doyo, alieleza kuwa chama hicho hakijaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ya "No reforms, no election". Badala yake, NLD itaendelea kuwaeleza wananchi sera zake.
"Vyama vya siasa vipo 19, ikiwemo NLD. Sisi hatuendi msituni wala hatususii uchaguzi, bali tunaenda kuwaeleza wananchi sera zetu ili watupe ridhaa ya kuwaongoza,"
Alieleza kuwa mwaka 2015, vyama vya NLD, CUF, CHADEMA, na NCCR-Mageuzi viliungana kwa lengo la kuiondoa CCM madarakani, lakini NLD ilidhurumiwa kwa kuwaondoa wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uchaguzi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa NLD, Mfaume Khamis Hassan, wakati akifungua mkutano huo, ameomba serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwapatia ajira za kudumu walimu wanaojitolea.
Aidha, Mwenyekiti huyo amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi na kuepuka vyama vya siasa vinavyohamasisha uvunjifu wa amani.
Katika hatua nyingine, Mfaume amempongeza Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akimtakia kila la kheri katika safari yake hiyo.
Source: Nipashe