Dodoma. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kufanya mkutano mkuu maalumu Machi 12 mwaka huu.Mkutano huo utakuwa kwanza kwa Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli baada ya kupokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake Jakaya Kikwete.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo amesema kuwa mkutano huo utafanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa chama."Mkutano unafanyika kufuatia mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya chama chetu yanayopelekea kufanyika kwa marekebisho makubwa ya kanuni na katiba ya CCM," amesema MpogoloNaibu Katibu huyo amesema mkutano huo pia utajadili na kupitisha marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012, pamoja na kanuni za Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.