Chalinze: Ndugu wazika maiti isiyo yao, ilisafirishwa kutoka Kilimanjaro na kuzikwa Kiislamu wakati ni ya Mkristo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,533
3,186
Ilikuwa mshtuko baada ya ndugu wa marehemu Steven Hamis Massawe (60) kufika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi na kuukosa mwili wa ndugu yao.

Tukio hilo lilitokea juzi, baada ya ndugu hao kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kuuandaa mwili kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika jana, lakini kumbe mwili wa ndugu yao ulishachukuliwa tangu Juni 26 na kuzikwa siku hiyo hiyo Chalinze, mkoani Pwani kwa imani ya Kiislamu.

Tukio hilo ni miongoni mwa matukio kadhaa ya kubadilisha mili ya marehemu yaliyotokea hivi karibuni, likiwamo la mkoani Mbeya ambako mwili wa mwanajeshi mstaafu, Watson Mwambungu ulikwenda kuzikwa Wilaya ya Busokelo baada ya kuchukuliwa na watu wengine Juni 15.

Tukio lingine lilitokea Mei 19 baada ya ndugu wa marehemu Melkior Ndambale kwenda mahakamani kuomba kibali cha kufukua mwili wa ndugu yao uliokuwa umezikwa kimakosa wilayani Kilos Mkoa wa Morogoro.

Katika tukio la sasa, marehemu Steven Massawe, aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Omarini Kibosho, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro alifariki Juni 24, mwaka huu nyumbani kwake na mwili kupelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mawenzi. Hata hivyo, Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Edna-Joy Munisi alipotafutwa kwa simu kuzungumzia tukio hilo, simu yake iliita bila kupokewa.

Jana, ndugu wa marehemu, Thobias Massawe alisema Juni 28, mdogo wa marehemu alikwenda Hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya kuhakiki mwili, lakini hakuukuta katika chumba cha kuhifadhia maiti, jambo lililoibua mshtuko.

"Mazishi yalikuwa yafanyike leo (jana) Alhamisi, lakini hakuuona mwili na baada ya kuutafuta bila mafanikio, alitoa taarifa kwa uongozi wa hospitali ambao walifanya ukaguzi na kujiridhisha mwili haupo.

"Walianza kufanya ufuatiliaji kujua mwili umechukuliwa na nani na ndipo walipobaini kumefanyika makosa, kwani marehemu mwingine anayeitwa Idd mwili wake umebaki mochwari na ndugu walichukua mwili wa Steven na kwenda kuuzika Chalinze," alisema.

Alisema ndugu wa Idd walichukua mwili tangu Jumatatu Juni 26 na pia ni Waislamu. "Walikwenda kuzika Jumatatu Chalinze na walizika kwa imani ya dini ya Kiislamu, huu uliobaki hapa si wetu, hivyo baada ya kugundua hivyo zikafanyika taratibu zikiwemo za kisheria kupata vibali, ili kwenda kuufukua mwili Chalinze," alisema.

Alisema kwa kushirikiana na ongozi wa hospitali, walichukua mwili wa Idd ulioachwa Mochwari wakaenda nao, ili kufanya taratibu za kufukua mwili wa Massawe na kuurudisha Kibosho Mkombole Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.
Aidha, alisema kwa sasa taratibu nyingine zinaendelea nyumbani kwa marehemu wakati wakiendelea kusubiri mwili wa marehemu, ili kuona kama utawahi kufika na kuuzika.

"Tukio hili limetusababishia hasara na usumbufu mkubwa, maana mpaka sasa hatuiui kama tutawahi kuzika leo licha ya kwamba maandalizi ya vyakula, vinywaji viliandaliwa na hata MC ameshalipwa na waombolezaji wamekaa kusubiri maziko ya mpendwa wetu," alisema.

Raymond Massawe ambaye ni kaka wa marehemu, alisema tukio hilo limeonyesha hakuna umakini katika eneo hilo na kuiomba Serikali kuwawajibisha wale ambao wamehusika na uzembe huo. "'Uzembe uliofanyika hapa Hospitali ya Mawenzi ni mkubwa na inaonekana hawako makini, kama mwili wa mtu utaletwa hapa, halafu ubadilishwe apewe mtu mwingine, wanaweza pia kubadilisha wa mtoto na kuchukua mtu mzima," alisema Massawe.
 
Ilikuwa mshtuko baada ya ndugu wa marehemu Steven Hamis Massawe (60) kufika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi na kuukosa mwili wa ndugu yao.

Tukio hilo lilitokea juzi, baada ya ndugu hao kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kuuandaa mwili kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika jana, lakini kumbe mwili wa ndugu yao ulishachukuliwa tangu Juni 26 na kuzikwa siku hiyo hiyo Chalinze, mkoani Pwani kwa imani ya Kiislamu.

Tukio hilo ni miongoni mwa matukio kadhaa ya kubadilisha mili ya marehemu yaliyotokea hivi karibuni, likiwamo la mkoani Mbeya ambako mwili wa mwanajeshi mstaafu, Watson Mwambungu ulikwenda kuzikwa Wilaya ya Busokelo baada ya kuchukuliwa na watu wengine Juni 15.

Tukio lingine lilitokea Mei 19 baada ya ndugu wa marehemu Melkior Ndambale kwenda mahakamani kuomba kibali cha kufukua mwili wa ndugu yao uliokuwa umezikwa kimakosa wilayani Kilos Mkoa wa Morogoro.

Katika tukio la sasa, marehemu Steven Massawe, aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Omarini Kibosho, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro alifariki Juni 24, mwaka huu nyumbani kwake na mwili kupelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mawenzi. Hata hivyo, Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Edna-Joy Munisi alipotafutwa kwa simu kuzungumzia tukio hilo, simu yake iliita bila kupokewa.

Jana, ndugu wa marehemu, Thobias Massawe alisema Juni 28, mdogo wa marehemu alikwenda Hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya kuhakiki mwili, lakini hakuukuta katika chumba cha kuhifadhia maiti, jambo lililoibua mshtuko.

"Mazishi yalikuwa yafanyike leo (jana) Alhamisi, lakini hakuuona mwili na baada ya kuutafuta bila mafanikio, alitoa taarifa kwa uongozi wa hospitali ambao walifanya ukaguzi na kujiridhisha mwili haupo.

"Walianza kufanya ufuatiliaji kujua mwili umechukuliwa na nani na ndipo walipobaini kumefanyika makosa, kwani marehemu mwingine anayeitwa Idd mwili wake umebaki mochwari na ndugu walichukua mwili wa Steven na kwenda kuuzika Chalinze," alisema.

Alisema ndugu wa Idd walichukua mwili tangu Jumatatu Juni 26 na pia ni Waislamu. "Walikwenda kuzika Jumatatu Chalinze na walizika kwa imani ya dini ya Kiislamu, huu uliobaki hapa si wetu, hivyo baada ya kugundua hivyo zikafanyika taratibu zikiwemo za kisheria kupata vibali, ili kwenda kuufukua mwili Chalinze," alisema.

Alisema kwa kushirikiana na ongozi wa hospitali, walichukua mwili wa Idd ulioachwa Mochwari wakaenda nao, ili kufanya taratibu za kufukua mwili wa Massawe na kuurudisha Kibosho Mkombole Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.
Aidha, alisema kwa sasa taratibu nyingine zinaendelea nyumbani kwa marehemu wakati wakiendelea kusubiri mwili wa marehemu, ili kuona kama utawahi kufika na kuuzika.

"Tukio hili limetusababishia hasara na usumbufu mkubwa, maana mpaka sasa hatuiui kama tutawahi kuzika leo licha ya kwamba maandalizi ya vyakula, vinywaji viliandaliwa na hata MC ameshalipwa na waombolezaji wamekaa kusubiri maziko ya mpendwa wetu," alisema.

Raymond Massawe ambaye ni kaka wa marehemu, alisema tukio hilo limeonyesha hakuna umakini katika eneo hilo na kuiomba Serikali kuwawajibisha wale ambao wamehusika na uzembe huo. "'Uzembe uliofanyika hapa Hospitali ya Mawenzi ni mkubwa na inaonekana hawako makini, kama mwili wa mtu utaletwa hapa, halafu ubadilishwe apewe mtu mwingine, wanaweza pia kubadilisha wa mtoto na kuchukua mtu mzima," alisema Massawe.​
Pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wa chumba cha maiti lakini kule ndani kuna vitu vingi vya ajabu kushangaza na mauzauza mengi
Muhudumu aliyeko zamu asipokuwa makini ni rahisi sana kuchanganyikiwa kwa muda na kuchanganya miili

Hizi maiti zinazochanganywa nyingi huwa na kasoro za kiroho, migogoro ya kifamilia na koo ama huitishwa na nguvu fulani huko zinakopelekwa kuzikwa kimakosa
Nimefanya kazi mochwari nayajua haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisema wawajibishwe Kwan ndugu waliofata maiti hapo hospitali hawajui ndugu Yao!?? Kwani hawakumuona!? Tatizo lipo Kwa wanaokwenda kuchukua maiti
 
Very interesting. Hao ndugu hawakuwa wanamjua ndugu yao? Ina maana hawakutambua maiti kabla ya kubeba na kuzika?
Hii nchi nzuri sana..mazingaombwe fulu fulu kila upande
 
Ndio ilikuwa hatima yake hiyo
Hapana. Hatima yake ni kuzikwa na ndugu zake. Turekebishe makosa kama haya kwa kuwa na mfumo mzuri wa utambuaji si maiti tu bali hata wagonjwa na watoto wanaozaliwa.

Ifike mahala tubadilike na tuache hizi kauli za ajali haina kinga, ilikuwa mapenzi ya Mungu, ndiyo ilikuwa hatima yake hiyo bali tuwajibike, turekebishe na tuhakikishe makosa yale yale hayajirudii kwa sababu zile zile.

Samahani kwa "kukuzodoa" nkoyi...๐Ÿ–๐Ÿ–๐Ÿ–๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ
 
Chikupendiii
 
Pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wa chumba cha maiti lakini kule ndani kuna vitu vingi vya ajabu kushangaza na mauzauza mengi
Muhudumu aliyeko zamu asipokuwa makini ni rahisi sana kuchanganyikiwa kwa muda na kuchanganya miili

Hizi maiti zinazochanganywa nyingi huwa na kasoro za kiroho, migogoro ya kifamilia na koo ama huitishwa na nguvu fulani huko zinakopelekwa kuzikwa kimakosa
Nimefanya kazi mochwari nayajua haya

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaan wewe umefanya vitu vya hatar hatar tu
 
Back
Top Bottom