Chalamila awasili Kariakoo awaambia Wafanyabiashara “Fungueni maduka, Biashara sio Siasa”

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,688
6,484
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefika soko la Kariakoo kutokana na Biashara kufungwa kuanzia leo Juni 24, 2024 na kuongea na wafanyabiashara.

Chalamila amesema wafanyabiashara wako wa aina kadhaa ikiwemo walioshiba, kati na wachanga na iwapo wataigana kuna watakaojuta leo, kesho na mwingine baaada ya mwezi mmoja. Chalamila amesema ni kweli wafanyabiashara wanaweza kuwa na changamoto lakini zipo nyingine za kisheria na haiwezaki kuzisuluhisha asubuhi na mapema.

photo_2024-06-24_11-56-48.jpg

Chalamila amesema duka si sawa na hospitali kwani hospitali zingegoma ingekuwa hatari zaidi na kuomba busara itumike. Mwisho amemaliza na mkwara mzito kwa yeyote atakaempiga mkwara aliyekubali kufungua.

"Aliyekubali kufungua afungue na yule ambae atamletea mkwara mtu yeyote yule aliyekubali kufungua naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonesha shoo nzima. Wewe unakuja unamletea mkwara, mimi nitakuchimba mkwara na hautaamka tena, na hili naomba niwaeleze ndugu zangu wa Kariakoo, utoto ukizidi hatuwezi kufikia hapo"

Pia Chalamila amewashukuru waliofungua maduka na kuwaahidi waliofunga atazilinda biashara zao na hakuna mwizi atakaeiba hata kama itakuwa mwezi. Chalamila amesema biashara sio siasa na leo jioni wataona hasara yake lakini siasa haiwezekani kugundua hasara zake.

Chalamila pia amedai yeye kama mkuu wa mkuu wa mkoa akiumua kwenda kukaa madukani kwao aangalie kiwango kikubwa cha ukwepaji kodi, amehoji kama wataweza kuishi Kariakoo!

Pia, soma=> RC Chalamila: Wafanyabiashara wa Kariakoo wajitafakari, migomo siyo suluhisho




photo_2024-06-24_12-03-49 (2).jpg

photo_2024-06-24_11-56-48 (2).jpg



 
Kamati kitu gani. Fungueni maduka Wananchi wapare huduma. Vinginevyo mtaishia kupata kipigo cha Mbwa mwizi
We utakuwa mjinga sana na hujui chochote,na ujinga kama wako ndiyo wanasiasa wanautumia,kama unawatoto wanakuita Baba basi wana Baba wa ovyo kabisa kuwahi kutokea duniani.Acha kukurupuka wewe na ukoo wako mnaathirika na mfumuko wa bei ya bidhaa acha ubwege
 
Back
Top Bottom