Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,840
- 47,501
Kama nchi, tupo katika hali mbaya sana, karibia katika kila eneo.
Siamini kuwa tukichagua wapinzani, mambo yatabadilika mara moja na kuwa mazuri. Uharibifu ufanywe kwa miongo mingi, halafu mabadiliko yalete mema mara moja, siyo jambo rahisi.
KWANINI NI BUSARA KUCHAGUA WAPINZANI.
1) CCM imejaa kiburi. Haisikilizi umma, haijali wala haina hofu katika lolote inalolifanya, kwa kuamini kuwa wananchi wote ni tutusa, hawana uwezo wa kuwatenda lolote.
2) Kuwachagua wapinzani na kuwafurusha CCM kutajenga hofu kwa watawala na vyama vyao vya siasa kuwa wakitenda wasioyataka wananchi au yenye kuwaumiza wananchi, wananchi hawatawavumilia, watawaondoa.
3) Kuwachagua wapinzani, kutatengeneza mazingira rahisi ya kupata katiba mpya, kujenga mifumo mizuri ya kiutawala, na kuondosha utawala holela ambao unamfanya kila Rais kujiamlia anayotaka kwa sababu hakuna mwongozo wa jumla kwa watawala.
4) Uchaguzi ni lazima usimamiwe na umma wenyewe. Isipofanyika hivyo, CCM kama kawaida yao, watawapuuza watanzania, kwa kuiba kura au kuwatangaza washindi wa uchaguzi wanawataka wao na sio wanaotakiwa na wananchi.
WANANCHI WATASIMAMIA VIPI UCHAGUZI?
Bila ya kujali sheria za kijinga zinazohamasisha wizi wa kura zilizowekwa na CCM, wananchi katika umoja wetu, wakati wa kampeni, tutangaze kuwa TUME YA UCHAGUZI IPO CHINI YA WANANCHI NA ITAWAJIBIKA KWA WANANCHI.
a) Wakati wa upigaji kura, kura zitahesabiwa mbele ya umma wote kwa kuonesha kura moja moja, na mwananchi yeyote atakayetaka kwa kuiangalia kura hiyo atafanya hivyo (kama wanavyofanya Nigeria). Baada ya ujumlishaji wa kura, pamoja na watendaji wa tume kutoa nakala ya matokeo, kubandika kwenye kituo cha kupigia kura, mwananchi yeyote atakayetaka, ataruhusiwa kupiga picha nakala hiyo ya matokeo. Wakati wote wa zoezi zima wananchi, watakuwa na uhuru wa kupiga picha na kuchukua video. Wakati wa ujumlishaji wa matokeo ya mwisho kwenye kila ngazi, tume itakuwa na sehemu yake ya kufanyia majumuisho, na wananchi waliochaguliwa na wananchi wenzao watakuwa na eneo lao la kufanya majumuisho. Kama matokeo ya ujumlishaji ya wananchi yakafanana na ya Tume, mshindi atatangazwa. Yakitofautiana, wananchi wataongeza wawakilishi wa kupitia ujumlishaji, na mwisho matokeo ya ujumlishaji wa wananchi ndiyo yatafuatwa, na msimamizi wa uchaguzi ALAZIMISHWE, APENDE ASIPENDE, LAZIMA ATANGAZE MSHINDI KWA KADIRI YA TAKWIMU ZILIZOJUMLISHWA NA WANANCHI.
Tunawachekea watu wanaozidi kuliangamiza Taifa la leo, kesho na kesho kutwa, ilihali hawana chochote cha pekee zaidi ya wizi, uwongo na ufisadi.
Pesa ya kigeni hakuna, umeme wa kubabaisha, hata sukari tu shida, kodi na tozo kila siku wakati watu wanateseka na kupambana na mazingira magumu ya uchumi yanayosababishwa na kutokuwepo kwa umeme wa uhakika, ufisadi, mipango mibovu, na uwongo wa watawala. Walisema umeme wa uhakika utaanza kupatikana mwezi February, sahizi wamebadili hadithi.
Ugoigoi wetu umelifanya Taifa kuwa goigoi. CHADEMA pamoja na maandamano ya kupinga sheria mbovu za uchaguzi na hali ngumu ya maisha, nendeni mbele zaidi, yaani kuwaandaa wananchi juu ya nini cha kufanya dhidi ya hao watawala wanaowadharau na kuwatesa wananchi, kwa wakati huu na wakati wa uchaguzi.