Chafya haiwezi kumzuia mpishi kuivisha pilau kuiva

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,803
Wanaume wengi wanapenda wanawake wazuri wenye mvuto ,shape nzuri na mavazi ya kuvutia mbele za watu ila wameshindwa kuwa na jicho la kuwatizama wanawake bora wenye tabia nzuri,haiba ya kike,mapenzi ya dhati,wavumilivu na wenye njaa ya kuitwa mama na mke bora.

Mwanamke bora ana sifa za mke bora sababu anampikia mume wake,anamfulia nguo mume wake,anamnyoshea nguo mume wake,anamshauri mume wake mambo ya msingi,hapendi pesa bali anachangia pesa katika ujenzi wa familia,anajua kulea watoto na mume wake kwa ubora wa hali ya juu na hapo ndipo wanaume huwa na wivu na wanawake hawa.

Wanawake wenye sifa za uzuri wa sura ,shape na mvuto mbele za watu wengi wao wana sifa za mahouse girl sababu hawawezi kupika,hawajui kufua nguo,hawawezi muandalia mume wake nguo za kazi wala kumuandalia chakula mume wake na ni mabingwa wa kuomba pesa na tegemezi kwa kila kitu.

Mwanaume mwenye upofu wa mawazo huwa anashindwa tofautisha katika ya mke mwema na mke mzuri,unaweza kuwa mzuri na usiwe bora ila unaweza kuwa bora na ukawa mwema na muadilifu ,kama wewe mwanaume una housegirl anayekupikia ,anakufulia nguo,anakuandalia chakula,anakuadalia maji ya kuoga na kukuheshimu basi jua huyo ana sifa zote za mke mwema ingawa ni house girl.

Kama una mke ambaye hapiki chakula,hawezi fua nguo,hawezi bembeleza mtoto ,hana mawazo chanya,na ni tegemezi bila kusahau anatumia muda mwingi kwenye social networks,anapenda kuchati sana na simu na anapenda kushinda saloon jua huyo sio mke ila ni demu na house girl wako ana sifa za mke sababu anafanya majukumu ya mke wako.
GedsellianTz
 
Nilikuwa na demu wangu mzuri mpole na ananipa mashauri mazuri sana lakini hajui kupika. Halafu nilipata huyu sio mzuri kihivyo lakini mpishi mzuri sana tumbo halilali na njaa tatizo lake ana kejeli mbaya sana. Sasa sijui yupi mke mzuri kati ya hawa wawili bila ya kusahau wote wana hold degree?
 
Huyo asiyejua kupika yakupasa umpe darasa la kupika mtafute dada ako unayeelewana nae amfundishe au mama ake mzazi amfundishe then utafurah mwenyewe....yawezekana hajui kupika lakini sio kosa lake mazingira yalimfanya awe hivo " ukipata kizuri kishikilie"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…