Chadema yapita njia ya ACT kuhusu Katiba Mpya

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
340
359
Wakati madai ya upatikanaji wa Katiba Mpya uliposhika kasi vyama tofauti vilitoa mapendekezo ya Nini kifanyike ikiwa nafasi ya upatikanaji wa Katiba hiyo Kabla ya Uchaguzi wa SERIKALI za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025 utakuwa haionyeshi dalili ya kufanikiwa.

ACT Wazalendo,katika maoni Yao walipendekeza kuwa mchakato wa Katiba ufanyike na uanze sasa huku vipengele muhimu kuelekea uchaguzi wa 2024 na 2025 vipelekwe bungeni kufanyiwa mabadiliko.

Vipengele vilivyopendekezwa kupelekwa bungeni na kufanyiwa mabadiliko ni namna ya kupatikana wajumbe na wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi,Sheria ya Uchaguzi na vyama vya Siasa pamoja na Sheria ya jeshi la Polisi.

Maoni hayo ya ACT Wazalendo yalipingwa kwa kiasi kikubwa na Chadema huku wakisema Chama hicho inakisaidia Serikali kukwamisha mchakato na wao waksinikiza kuwa ni lazima Katiba ipatikane na isipopatikana hawatashiriki Uchaguzi.

Kila walivyoelekezwa na ACT na hata Peter Kibatala alizoeleza katika Moja ya maoni yake umuhimu wa kuwa na Tume huru Kabla ya Katiba Chadema waliendelea kukunja ngumi na kusema Katiba itapatikana Kwa nguvu ya Umma bila kuainisha hatua gani zianze

Leo katika mkutano wao na waandishi wa Habari Kupitia Kwa Suzan Lyimo,Chama hicho Cha muda mrefu kimebeba mawazo ya ACT Wazalendo na kutaka baadhi ya vifungu viende bungeni kufanyiwa mabadiliko Kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi mkuu utakaokuwa na Tume huru

Zitto Kabwe mara kadhaa katika kuchangia mijadala ya kitaifa alikuwa anawaonya viongozi wenzie wa kisiasa kuwa wasipoongoza wataongozwa

Ama kweli nimeamini ACT ni Chama kiongozi na viongozi wao ni Twiga wenye kuona wengine wasipoona

Kula Chuma chini msikilize Lyimo Suzan
 
Back
Top Bottom