Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,395
- 6,617
Wakuu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemwandikia barua Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mwanga, Lembruce Mchome kikimtaka ajieleze ndani ya siku 14 kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu.
Mchome ameingia kwenye mgogoro na chama chake baada ya kuhoji uhalali wa akidi ya kikao cha Baraza Kuu ambacho kilichothibitisha uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Soma: Msajili wa Vyama vya Siasa aipa wiki moja CHADEMA ijibu barua ya Mchome
Februari 18, 2025, Mchome aliandika barua ya malalamiko kwa katibu mkuu akipinga uteuzi uliofanywa na mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, wa viongozi wa juu wa chama na wajumbe wa kamati kuu kwenye mkutano wa Baraza Kuu Taifa uliofanyika Januari 22, 2025.
Kada huyo ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu alipeleka nakala ya barua hiyo kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na baada ya ukimya wa siku kadhaa, alikwenda kulalamika kwa Msajili, akitaka majibu ya barua yake na Msajili aliielekeza Chadema imjibu ndani ya wiki moja, kabla ya Machi 31, 2025.
Leo, Machi 26, 2025, Ofisi ya Katibu wa Chadema Kilimanjaro imemwandikia barua Mchome kwa mujibu wa katiba ya chama ya mwaka 2006 toleo la 2019, Maadili ya Viongozi 10.1(vi), 10.2 (ix) na Maadili ya Wanachama 10.3 (iii) ikimtaka maelezo.
Chanzo: Mwananchi