CHADEMA wana kazi kubwa ya kuwapata Katibu Mkuu na Mgombea Urais 2020

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,388
Wadau, amani iwe kwenu.

Ni dhahiri kwamba Uchaguzi Mkuu wa 2015 umemalizika. Kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa 2015 kunatoa fursa kwa vyama vya siasa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Mpaka sasa, ni chama cha Mapinduzi pekee ndicho hakina ombwe la Uongozi. Labda wanafuatia ACT. Ila kwa CHADEMA na CUF wao wana shughuli pevu ya kujaza mapengo yaliyoachwa wazi kutokana na viongozi wake wakuu kuachia ngazi baada ya kubakwa kwa mfumo wa kumpata mgombea Urais kupitia UKAWA.

Hata hivyo, CHADEMA wana kazi kubwa mbili mbele yao. Kwanza kumpata Katibu Mkuu ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Dk Slaa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Julai 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, nafasi hiyo ilipaswa kujazwa ndani ya siku tisini. Hata hivyo mpaka sasa, nafasi hiyo ipo wazi na taarifa zilizopo ni kwamba CHADEMA wamekosa mtu mwenye sifa za kukaribia sifa za Dr Slaa. Kutokana na kukosa mtu ndani ya CHADEMA, chama hicho kikawa na wazo la kumteua Frederick Sumaye kushika nafasi hiyo. Hata hivyo, mapendekezo hayo yanakataliwa na baadhi ya Mahafidhina.

Kazi ya pili ni ya kumpata Mgombea Urais. Ni dhahiri kwamba Edward Lowasa hatakuwa mgombea Urais wa CHADEMA kwa mwaka 2020. Kwani mpaka sasa, imedhihiri kuwa mwanasiasa huyo ameshapoteza mvuto na mwelekeo. Ndani ya CHADEMA mpaka sasa hakuna figure hata moja ya kuivusha CHADEMA 2020. Jicho lao limeangaza tena kwa Sumaye. Hata hivyo, bado hali ni tete kwani Sumaye hana umaarufu wa kumzidi Lowasa. Hivyo kama Lowasa alipigwa kirahisi na Magufuli, sijui kwa Sumaye hali itakuwaje.

Pupa, ulafi na tamaa ya Mbowe ndiyo imewafikisha hapa CHADEMA.
 
kwanini unapenda kuwaongelea chadema mmno, waache na mambo yao, nenda mtindo wa ccm, kwa sasa achana na chadema, unaonyesha una chuki sana!!
 
huyu mbulula huwa simuelewi hasa anatafuta nini kwa chadema, vyama vya siasa vipo vingi nchini ni zaidi ya 10 lakini yeye chademaa chadema
 
kwanini unapenda kuwaongelea chadema mmno, waache na mambo yao, nenda mtindo wa ccm, kwa sasa achana na chadema, unaonyesha una chuki sana!!
Kwa kawaida si kuwa nawaongelea bali naandika facts za ndani ya chama hicho
 
kwanini unapenda kuwaongelea chadema mmno, waache na mambo yao, nenda mtindo wa ccm, kwa sasa achana na chadema, unaonyesha una chuki sana!!
Mbona mnaongoza kufuatilia mambo ya Ccm kuliko Cdm!?
Kipindi cha Kukata watu Dodoma Hadi panya Wa Mbowe mlikodolea macho,masikio Kwa Ccm Inakuwaje
 
Unawaonesha mabwana zako wakuone

Msukule bwana.
Umejitutumua kweli kweli unaona umeandika

Chukua kadi ya M4C uwe katibu mkuu wewe.
Kwani sasa chadema inaendeshwa na M4C au 4 U Movement?? Chama ishauzwa hiyo M 4 C na redi brigedi hamna chenu hapo
 
Chadema tuliyoipenda haina tena mvuto imekuwa ni aibu hata kujitambulisha ww ni CDM. Uchaguzi ujao utakuwa mgumu mno hasa kwenye kutetea nafasi za ubunge wengi wataangukia pua.
Mwenye macho haambiwi tazama.
Wengi wanaishi kwa ushabiki
hawataki kuambiwa ukweli,
Chadema ina ongozwa hovyohovyo Na hakuna kuhoji,
siasa za kishabiki Na kufuata Mkumbo ndio kinga kuu ya Cdm Na viongozi wake, hili nitatizo
 


Mtafutieni pakuishi yule Mwenyekiti wenu kwanza
 
Wengi wanaishi kwa ushabiki
hawataki kuambiwa ukweli,
Chadema ina ongozwa hovyohovyo Na hakuna kuhoji,
siasa za kishabiki Na kufuata Mkumbo ndio kinga kuu ya Cdm Na viongozi wake, hili nitatizo
Na bado kuna mijitu itakuja hapa kutetea ujinga utadhani akili zao zina kideri cha bata. Nchi yeyote inahitaji upinzani ulio imara na sio huu wa akina mbowe kuangalia wanapata nini kuneemesha mifuko yao.
 
Huyu jamaa kiwalisia ni ccm hila anatamani kuwa chadema usijifiche kwenye maneno fanya mahamuzi amia chadema tu kuliko kijifanya msemaji wa chadema
 
Nakushangaa sana kuhusu mgombea wagombea ni wengi ndani ya ukawa .....katibu mkuu haina haja kuwa naye anayekaimu anatosha...
 
@Lizaboni
===>Kasi ya magufuli ni kubwa sana,nafikiri JPM ni zaidi ya zile siasa za upinzani,ila mungu amjalie maisha marefu rais wetu
 
Nauhakika hata wewe mwenyewe ukirudia kusoma post yako hutaelewa ulichoandika
Ungekua hujaelewa usingejibu ila umejibu inamaana umeelewa.

Tatizo lenu nyie akili zenu hazina uwezo wa kufikiri

Ya kuna watu wana fikiri kwa niaba yenu.
 
Ungekua hujaelewa usingejibu ila umejibu inamaana umeelewa.

Tatizo lenu nyie akili zenu hazina uwezo wa kufikiri

Ya kuna watu wana fikiri kwa niaba yenu.
Haya nimekuekewa ...ila bado nasubiri jibu...Kwasasa chadema iko chini ya uongozi wa M4C au 4 U Movement...maana kuna story kuwa chama kimeuzwa
 
Hapa ndo ninapochoka na wewe na kukuona kwamba unalipwa kwa utumbo huu unaoufanya
Nilitegemea sa hvi uwe busy kukishauri chama chako na serikali yake sasa upo busy na CDM
 
@Lizaboni
===>Kasi ya magufuli ni kubwa sana,nafikiri JPM ni zaidi ya zile siasa za upinzani,ila mungu amjalie maisha marefu rais wetu
Ni kweli Mkuu. Wapinzani wana kazi kuhwa ya kujipanga. Jinsi Magufuli anavyotekeleza majukumu yake hawakudhani kama angefanya hivi. Amerejesha matumaini ya waliokata tamaa na CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…