SI KWELI CHADEMA waandika barua ya kusitisha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Salaam Wakuu,

Nimekutana na Barua hii mtandaoni, nasikia CHADEMA wametema bungo wanataka kujitoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa. Kuna ukweli hapa?

SI KWELI CHADEMA,,.jpg
 
Tunachokijua
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha upinzani nchini Tanzania, kilichoanzishwa mwaka 1992. Kinajulikana kwa kusimamia demokrasia, haki za binadamu, na utawala bora. Kimekuwa mpinzani mkubwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi mbalimbali.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni mchakato wa kidemokrasia ambapo wananchi hupiga kura kila baada ya miaka mitano kuwachagua viongozi wa ngazi za mitaa kama vile Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, na Wajumbe wa Serikali za Mitaa. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Tanzania kwa Mwaka huu unatarajiwa kufanyika November 27, 2024 (Soma hapa).

Leo Oktoba 10, 2024 kumeibuka barua yenye Nembo ya CHADEMA yenye taaifa inayoripoti kuwa Chama hicho kimekutana kwa Dharura kwenye kikao kinachodaiwa kuwa chini ya Freeman Mbowe na kukubaliana kutoshirki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27, 2024. Barua hiyo hapo juu inaonesha kusainiwa na kuandikwa ikionekana kuandikwa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na mambo ya nje John Mrema.

Je, Ukweli wa barua hiyo ni upi?
JamiiCheck Imefuatilia taarifa hiyo kwa kuitafuta kwenye kurasa rasmi za za CHADEMA ambapo tumebaini barua hiyo haijawahi kutolewa na CHADEMA kupitia kurasa zao Rasmi za mitandao ya kijamii wala kwenye vyombo vyake rasmi vya kutolea taarifa.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imewasiliana na Apollo Boniface Margwe ni Mkuu wa Idara ya Mitandao ya Kijamii wa CHADEMA pamoja na John Mrema ili kupata uhalisia wa barua hiyo, wote wamethibitisha kuwa barua hiyo sio yao na taarifa ya CHADEMA kujiondoa kushiriki Uchaguzi wa Seriklali za Mitaa haina ukweli.

Aidha, muda mfupi baada ya kuwasiliana na JamiiCheck John Mrema ameitumia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa X kuchapisha kanusho na kueleza kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na kuwataka watu kuipuuza. Tazama hapa chini:

1728595994263-png.3121396

kanusho la John Mrema kuhusu barua hiyo
CHADEMA na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa mnamo Oktoba 9, 2024 Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo (CHADEMA) John John Mnyika alifanya Mkutano na Waandishi wa Habari (huu) akisisitiza Wanachama wa CHADEMA kujitokeza na kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 (Soma hapa). Mkutano huo wa Mnyika unaasharia kujizatiti kwa chama hicho katika kushiriki Uchaguzi huo tofauti na ujumbe uliobebwa na Barua hiyo hapo juu.
Nashindwa kuelewa hawa Chadema hata nguvu ya kutamka uchaguzi inatoka wapi wanachama wako wanauliwa na wengine wanatekwa na kupotezwa na hawajulikani hadi waleo kwanini wasingeshughulika na hilo kwa hadi kieleweke..

Kwanini watu hawawajibishwi kwa madhira yanayotokea ya kupokonya watu uhai wao bila sababu za msingi.
Maana kama vyombo vinavyosimamai haki nchini pia haviaminiki basi kuna namna ya kufanya huko nje ya nchi pia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom