Wana chadema/UKAWA hivi ni kweli mna nia ya dhati ya mapambano dhidi ya ccm?
Ni wakina nani wanaunda chadema? Lengo lao la dhati ni lipi hasa? Kuna kipindi nawaona chadema kama mamluki wa ccm au kama wanajitegemea basi ni kama genge la watu Fulani ambao labda hata ndoto zao hazifanani na za watanzania wengi wanaoaminishwa wapo pamoja! Ni ngumu kujua malengo ya magenge mengi na kwa bahati mbaya wapo watu wanaoweza kujituma ktk makundi ya jamii kuwa wapo naive na wanataka mabadiliko ya kweli, lkn hao ni kwa ajili ya decoy tu, Ila wapo kweli ambao ni mbumbumbu kama Mimi ambao hawajui hila za hawa mabwana wakubwa!
Hebu tujaribu kuona nia njema za chadema!
- Chama hakina ofisi yenye ulinganifu na ukubwa wake, yaani hakuna wa kujitolea kukijenga kwa michango yao kama ilivyofanywa na TANU ingawa kuna watu wanaonasibiwa kwa kuwa ni matajiri sana kama Lowasa au Mbowe na Ndesamburo/Mtei au basi hata kwa matumizi ya ruzuku!
- Kwa kadri muda unavyoenda chama kinakomaa lkn sio nafasi yake ya uongozi wa juu. Imekuwa kama ufalme ni ukoo mmoja tu wenye privilege ya kutawala na kama huna affiliation nao basi uñakuwa threat. Zitto, Slaa, Chacha, Kitila na Kaborou wanaweza kuwa mifano! Lkn pia tabia ya kukumbatia weak politicians nayo inashangaza zaidi! Mtu wa propaganda kuwa Salim Mwalimu ambaye nadhani wakati wa kampeni zilizopita alikuwa anapambana na kina kinana na Nape!
- Chadema ilipaswa kujenga misingi ambayo ndio ingakitambulisha kwa wananchi, kama TANU ilivyokuwa ndani ya mioyo ya watanzania mafukara waliojichangisha kwa kila hali kwa kuwa walikuwa wanawekeza katika chama chao! Lakini hapana, kimantiki ni ngumu kuitofautisha ccm na chadema kwa aina ya watu waliopo pande zote 2, mipango ya vyama vyote kutumia wizi wa kura, kudanganya watu na kutumia mbinu nyingine chafu!
Natamani kufahamishwa juu tofauti za kimkakati, dhamira, usafi na jambo lolote la kisiasa au kimaendeleo ambalo chadema wamekuja nalo kama ndio chachu na dira ya mabadiliko kwa watanzania!
Otherwise napata shida kuona kwanini mtu aiache ccm na kuchagua chadema hasa ukitazama uwekezaji wa vyama hivi kama vifuatavyo:-
Lumumba/Chamwino vs Ufipa
Magufuli vs Lowasa
kinana vs kivuli****
Nape vs Salim Mwalimu??
Mbowe vs Kikwete
Wazee
Mwinyi, Warioba, Salim, Mkapa, etc vs Mtei, Kingunge, Ndesamburo, Makani etc
Chadema think bigger, mnaweza msitegemee sana aina ya watu mlionao kutokana na umaarufu, wekezeni katika character!
Jengeni chama chenye muelekeo lkn msiwe wababaishaji! Or else wekeni dhamira yenu ya dhati hadharani ili watu wajue kwanini wawachague!
Vipo vyama vyenye malengo tofauti duniani na watu bado wanavichagua kutokana na msimamo yao! Trump anapewa support US leo kwa misimamo yake, just kuweni bayana tutawachagua kwa hiyari yetu!