KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 88
- 166
Juzi zoezi la andikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, limehitimishwa kwa serikali kujipa kongele kubwa kuwa wananchi wengi wamejiandikisha.
Sasa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Simiyu kimesema kuwa katika zoezi hilo wamegundua uwepo wa hujuma ambazo zilifanywa na wasimamizi wa uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa Wa Simiyu Mussa Onesmo anasema kuwa baada ya zoezi kumalizika, mawakala wao waliandika jumla ya idadi ya watu ambao waliandikishwa kwa siku zote pamoja na kuandika jina la mtu wa mwisho aliyeandikishwa.
…… Vituo vyote tuliweka mawakala, na siku ile ya mwisho mawakala wetu wote kila kitu walikuwa wanaandika jumla ya watu walioandikishwa, lakini pia tuliwaelekeza waandike jina la mtu wa mwisho kuandikishwa…..
Amesema kuwa baada ya zoezi kukamilika, na kesho yake majina kubandikwa, wamebaini uwepo wa hujuma kubwa kufanyika, ambapo wamekuta kuna majina mengi zaidi yameongezwa ambayo ameadai kuongezwa kinyemela na waliofanya hivyo ni wasimamizi.
Mwenyekiti huyo anasema hayo majina ni hewa na yaliongezwa usiku, kama mjama za kutaka chama Fulani kishinde. Na hizi njama wamefanya wasimamizi eti.
Namnukuu kwenye video ambayo nimeona kwenye mitandao ya kijamii Global tv online anasema…Sisi tuna takwimu zote za kila kituo, na tuna jina la mtu wa mwisho kila kituo, lakini tumekuta majina mengi zaidi hewa kwenye vituo vingi, hili tumesema hatutalikubali hata kidogo, hakuna jina hewa litapiga kura, tutapambana nao…,” anasema..
Soma Pia:
- Mwanza: Karani abanwa baada ya kuongeza majina hewa 200 kwenye daftari la Wapiga Kura
- Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Video
Mwenyekiti huyo ametaja mitaa baadhi akisema kuwa hujuma imekuwa kubwa, ambapo alieeleza kuwa mbali na hatua nyingine, lakini chama hicho kitakata rufaa kwa mujibu wa sheria ili majina hayo yasipige kura.
Anasema …..Tunajua hizi ni hujuma za kutaka kupata ushindi kwa chama Fulani, sisi awamu hii hatutakubali na wala hatutasusia uchaguzi, tutachukua hatua zote majina hayo yasipige kura, tumeanza taratibu na kuyakatia rufaa,”..
Nimeona kwenye hiyo taarifa msimamizi wa uchaguzi ambaye ni ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Adrian Jungu, akiwataka viongozi hao kuacha kulalamika kupitia vyombo vya Habari na badala yake wapeleke malalamiko yao kwenye kamati za rufaa ili yapatiwe ufumbuzi.
“ Kanuni za uchaguzi huu ziko wazi kabisa, kuna kamati za rufaa kwenye ngazi ya kata na mitaa au vijiji, tunawaomba ambao wanalalamika wapeleke kwenye hizo kamati malalamiko yao, wasiishie kulalamika tu wapeleke hayo malalamiko kwenye sehemu husika,
Nimweka Link hapo chini wasikilize viongozi wa Chadema Mkoa wa Simiyu.
Chanzo: Global TV Online