kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 14,095
- 14,627
Kuna vitu vizuri na vibaya ambavyo watanzania wanavijua kuhusu CCM, Serikali, viongizi na Katiba yao, lakini wananchi bado wanaona kuwa mazuri bado ni mengi kukiko mabaya yao.
Ndio maana bado watu wanavaa mashati ya kijani mitaani bila hofu. Watanzania pia wanafahamu mazuri na mabaya ya vyama na viongozi wa upinzani lakini bado wanaona mabaya yao ni mengi kuliko mazuri, ndio maana mitaani kuko shwari hata kama viongozi wa upinzani wakikutana na masahibu gani ya kisiasa.
Na hii inatokana na viongozi wa upizani kuwa na tabia ya kuorodhesha matatizo tu bila kusema wao watafanya nini kuyaboresha katika mazingira kama haya ya dunia ilivyo. Kuna wakati wapinzani wanarudi CCM kila wakinyimana maslahi kuonyesha kuwa dhamira zao ni maslahi yao tu sio shida za wananchi orodha ya wapinzani waliorejea CCM ni ndefu sana na inayokatisha tamaa wananchi kuviamini vyama hivi kama vyama kimbilio kwao.
Kama utadhani kuwa hakuna watu wameichoka CCM utakuwa unakosea tena sana. Inafahamika kuwa ccm imekusanya watoto wanaccm wa zamani na sasa kuwapa zawadi na fadhila za kutuongoza hata kama wengine hawana uwezo wa kuongoza. Lakini hawaoni nani wa kumpa uongozi mbadala wa ccm bado.
Kuna kiongozi wa upinzani unasema naaam huyu ni madhubuti, lakini mara utasikia ameenda au amerudi ccm.