CHADEMA ni kwanini mnauwa demokrasia ya vyama vya upinzani?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Ni vigumu kuamini lakini kuna uchunguzi nimeufanya nikagundua chama cha CHADEMA tangu mwaka 2010 kilipopata nguvu kimekuwa kikifanya siasa ya kuua vyama vingine vya upinzani pamoja kuua agenda za upinzani hapa Tanzania kwa kutilizama hilo jambo hebu tuangalie mfumo wa siasa tangu 2010.

1.Mwaka 2010 baada ya uchaguzi mkuu kumalizika CHADEMA waliwahi kuwatuhumu CUF chini ya Maalim Seif kuwa CUF ni CCM B imeolewa na CCM.

2.Mwaka 2013 CHADEMA waliwahi kuwaita CUF chama walibelelari hadi ukazuka mtafaruku kupitia bungeni.

3.Mwaka 2014 baada ya NCCR kuteuliwa kwa Mbatia kuwa mbunge na JK kuna wana CHADEMA waliwahi kusema mbatia ni CCM na sio mpinzani.

4.Mwaka 2015 baada ya CUF, NCCR, NLD kuungana na CHADEMA mwisho wa siku chama cha NCCR, NLD vilikufa kupitia UKAWA baada ya kuungana na CHADEMA.

5.Mwaka 2015 chama cha CUF ambacho kilikuwa na nguvu jimbo la Segerea kilimalizwa nguvu na CHADEMA baada ya kuwekea mgombea.

6.Mwaka 2016 CHADEMA baada ya Lipumba kurudi CHADEMA wamekuwa wakifanya siasa za kumtuhumu Lipumba asirudi CUF ili mradi CUF vife.

7.Mwaka 2016 hawakuishia hapo sasa hivi nguvu nyingi wanazielekeza ACT ili kukimaliza nguvu ili kuhakikisha ACT haipandi chati na juzi juzi walishaandika chama cha zitto kinadaiwa.

Leo hii tunaelekea uchaguzi wa kata 22 CHADEMA kasimamisha wagombea kata zote sasa hapa ndipo najiulizaa hivi UKAWA uko wapi?

Na je nini hatma ya NLD, NCCR na CUF ndani ya UKAWA.
 
ndo maana mbowe akiona kiongozi wa chama cha siasa mwenye akili ya kuhoji, mfano, prof Lipumba, Mh Zitto anawapiga vita sana, anawapenda viongozi mazuzu kama maalim, kina mbatia hii ni hatari sana
 
Chadema wanaoshinda wakitukana wenzao kuwa ni ccm b, Alafu mwaka 2015 chadema hao hao wakachukua makapi ya ccm kugombea urais!!!!!

Ama kweli shetani akizeeka huitwa malaika.
 
Usiwaamini wanasiasa..ni waongo na wanafiki..lengo la wanasiasa ni kupata cheo tu.chadema ni walewale. Ishu ya mtatiro na atropia ilidhihirisha upuuzi wa chadema. Chadema wapo kimaslahi tu.
 
Una uhakika na maneno tmia akili kbla hjapost HV inaingia akilin lengo LA chadema ni kumzuia lipumba ni kuua upnzan acha acha ushabik maandaz ktka siasa ,, MTU aljtoa mwnywe uenyekti chdema htoa ushaul kwa cuf ili imzuie lipumba asilete mtafaruko ukawa tmia akili kupost
 
ndo maana mbowe akiona kiongozi wa chama cha siasa mwenye akili ya kuhoji, mfano, prof Lipumba, Mh Zitto anawapiga vita sana, anawapenda viongozi mazuzu kama maalim, kina mbatia hii ni hatari sana
mkuu nakuunga mkono katika hiloo
 
Chadema wanaoshinda wakitukana wenzao kuwa ni ccm b, Alafu mwaka 2015 chadema hao hao wakachukua makapi ya ccm kugombea urais!!!!!

Ama kweli shetani akizeeka huitwa malaika.
hahaaaa tena nimeipenda sana hii hojaa wao walichukua mgombea toka ccm hilo halina ubishii
 
hapo kwenye namba 6......una shida ya displacement ndugu yangu.
 
C programming, Bila kusoma content za andiko lako, heading yako inaonyesha uwalakini wa ufahamu wako wa nani hasa anayekandamiza na kuua demokrasia Tanzania. Na usipojua ADUI unayepigana nae, utapigana vita visivyo sahihi.

C programming
 
mkuu ni ukweli upi unautaka wewe wakati mambo hadharani yanajulikana ni ni chama gani kinauwaa upinzanii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…