Pre GE2025 CHADEMA na wadau wengine kuishtaki Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
851
1,726
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema chama hicho kwa kushirikiana na wadau wengine, kiko kwenye mchakato wa kwenda mahakamani kuishtaki Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Lissu, mtaalam wa sheria na mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, amesema lengo lao ni kuzuia mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ukiwamo ugawaji majimbo uliotangazwa hivi karibuni na INEC.

Alibainisha hayo jana wakati wa mahojiano maalumu na waandishi wa habari wa gazeti la Nipashe na Nipashe Digital, nyumbani kwake Tegeta mkoani Dar es Salaam.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Lissu alisema tayari mchakato huo uko tayari na wakati wowote watakwenda mahakamani.

"Kwanza kwenye hiyo ya tume kuanza mchakato wa kutengeneza majimbo upya, tunafungua kesi Mahakama Kuu kwa kushirikiana na wadau wengine kama Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), na mimi nimesaidia kudrafti hiyo kesi, kuomba itamke kwamba huo mchakato ni haramu, iupige marufuku.
 
Kina kitenge na Hando wanasema huko ni kupoteza muda, wanadai kabla hata hukumu haijtoka watu watakuwa wameshaapishwa, wanadai wana CDM wanataka kushiriki hawatakubaki kususia ila Lissu anawahadaa.
 
Sijui kama wameliona hili, katiba ya Jamhuri ya Muungana wa tanzania ibara ya 75(6) Bila kujali masharti mengineyo ya ibara hii, hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume katika utekelezaji wake wa kugawa Jamhuri ya Muungano katika majimbo ya uchaguzi.

Hili haliwaondolei uwezo wa kufungua shauri?
 
Back
Top Bottom