Chadema na kitanzi cha People’s power Mbeya

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jiji la Mbeya kiko njia panda, kusimamia sheria au kufurahisha wafanyabiashara wadogo ‘wabishi’.

Chama hicho kimejikuta kwenye mkanganyiko huo kutokana na vurugu za wafanyabiashara hao, zilizotokea asubuhi ya Jumamosi iliyopita na kusababisha uharibifu mkubwa wa Barabara Kuu iendayo nchi jirani ya Zambia, baada ya kukuta vibanda na bidhaa zao zimeharibiwa na watu wanaoamina ni askari Jiji.

Baada ya wafanyabiashara hao kufika eneo lao la kazi na kukuta vibanda vikiwa vimevunjwa na bidhaa kukanyagwa na kuporwa, walifunga barabara kuu inayopita eneo hilo la Mwanjelwa kuelekea nchi jirani ya Zambia kwa kurundika mawe na kuchoma magurudumu ya magari.
Vurugu hizo za machinga zimesababisha uharibifu mkubwa kwa barabara hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi, kutokana na kuunguzwa kwa lami yake.

Taarifa zilizovuja kutoka Chadema Jiji la Mbeya, zinabainisha chama hicho kuchanganywa na vurugu hizo na kwamba ilikuwa wajadili jambo hilo katika kikao chao cha Jumatatu wiki hii.
Chanzo chetu kinaeleza kuwa kinachowachanganya zaidi katika kulikabili tatizo hilo ni Baraza la

Madiwani la jiji hilo ambalo linaongozwa na Chadema kutolijadili suala la kuwaondoa machinga hao kutoka katika eneo hilo la Kabwe, lakini wakati huo huo ikifahamika wazi kwamba machinga hao hawapo kisheria katika eneo hilo na kwamba wanafahamu kuwa wanatakiwa kuondoka na kuhamia kwenye eneo walilotengewa na jiji.

Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi, hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kwa undani akisema wanakutana Kamati ya Fedha ambapo baada ya kikao chao ndipo wataweza kuwa na kauli kuhusu mgogoro huo.

Raia Mwema lilipotaka kufahamu kuhusu athari za mgogoro huo kwa chama chake, aliomba kusubiri majadiliano ya kikao, hata hivyo alisema; “Yote yanawezekana, tutayaangalia kwenye kikao, lakini nina imani hekima ya wengi itaamua.”

Vurugu za wafanyabiashara hao, maarufu kama machinga, zilitokea kwenye kituo cha mabasi madogo yanayofanya safari zake ndani ya Jiji hilo, Kabwe, kilichopo katika eneo maarufu la kibiashara la Mwanjelwa.

Jeshi la Polisi lilizima vurugu hizo, baada ya kupeleka kikosi cha kuzuia fujo (FFU) wakiwa na gari lenye maji ya kuwasha. Hata hivyo, tofauti na ilivyozoeleka, jeshi hilo halikutumia nguvu wala mabomu ya machozi, walidhibiti kwa kuwatuliza wafanyabiashara hao wasifanye uharibifu.

Mashuhuda wa vurugu hizo, wanaeleza kuwa zilianza asubuhi, pale wafanyabiashara hao walipofika eneo lao la kazi na kukuta vibanda na bidhaa zao zimeondolewa na baadhi zikiwa zimesambaa chini baada ya kuvunjwa kwa vibanda vyao.

Askari wa Jiji, walioendesha uvunjajii huo, wanadaiwa kuvunja vibanda, kupora bidhaa za wafanyabiashara hao na kufanya uharibifu wa baadhi ya bidhaa.

Wafanyabiashara hao wamekuwa na kawaida ya kuacha bidhaa zao kwenye maeneo yao ya biashara, na kitendo cha askari hao wa Jiji kuvamia usiku na kuviondoa pamoja na bidhaa zao, iliwasababishia hasara na kuathiri mitaji yao.

“Askari wa Jiji walipita usiku, walivunja vibanda vya machinga na kuharibu bidhaa zao, walikanyagakanyaga na vingine walichukua, kitendo hicho kiliwaudhi machinga, ndipo nao wakaanzisha vurugu,” anasema mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo la Kabwe aliyejitambulisha kwa jina moja la Neto.

Uongozi wa Jiji hilo unalaumiwa kutumia mbinu ya kuvizia usiku wakati wahusika hawapo eneo la tukio na kufanya uharibifu na uporaji wa mali.
Machinga wadai kutokuwa na taarifa

Baadhi ya wafanyabiashara hao wamedai kuwa waliamua kufanya vurugu kutokana na kitendo cha askari wa jiji kuvamia eneo hilo na kuvunja vibanda vyao, kuharibu bidhaa kwa kuzikanyaga na hata kupora.

Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao waliozungumza na Raia Mwema eneo la tukio, hawakuwahi kujulishwa kuhusu kuondoa bidhaa zao, bali walichoelezwa ni kuhusu kufanya usafi kwa mujibu wa ratiba ya kitaifa ya Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi.

Pamoja na siku hiyo ya mwisho wa mwezi kutengwa kwa ajili ya usafi, wafanyabiashara hao wanadai nao kuwa na utaratibu wao wa kufanya usafi kila siku ya Jumatano na Jumamosi, na kwamba kila mfanyabiashara anawajibika kuwa na chombo cha kuhifadhia taka kwenye eneo lake la biashara.

Msimamo wa Jiji
Hata hivyo, ukweli ambao hauwekwi wazi na wafanyabiashara hao pamoja na baadhi ya viongozi wa Chadema jijini humo, ni hatua ya wafanyabiashara hao kuuza maeneo yao waliyopewa na jiji katika eneo la Kituo cha Mabasi yaendayo nje ya jiji na mkoa, cha Nanenane.

Kaimu Mkurugenzi Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro aliliambia Raia Mwema kuwa hata machinga wenyewe wanaelewa kuwa hawapaswi kuwepo eneo hilo la Kabwe na barabara iendayo kwenye Kituo cha Afya kilichopo, jirani na Soko jipya la Mwanjelwa.

“Walishapewa eneo Nanenane, wakauza kwa wafanyabiashara wakubwa, serikali ilitekeleza wajibu wake kuwasaidia,” anasema Dk. Lazaro.

Msimamo wa uongozi wa jiji hilo ni kwamba kazi hiyo ya kuwaondoa moja kwa moja machinga kwenye maeneo hayo ya vituo vya mabasi na kwenye barabara iendayo kwenye kituo cha afya itaendelea na kwamba walikwishatangaziwa kabla ya kuanza kazi kwa hiyo ili waondoe bidhaa zao.

Lengo kuu la msimamo wa jiji hilo ni kudumisha usafi na kuondoa msongamano kwenye maeneo muhimu kama yale ya kutolea huduma za afya.

Jiji hilo limeamua kutumia utaratibu wa kuwaondoa machinga usiku kuepusha usumbufu na vurugu ambazo hutokea wanapofanya kazi hiyo mchana.

Hata hivyo, utaratibu huo unapingwa na baadhi ya wakazi wa Mbeya wakisema unasababisha hasara kwa wafanyabiashara kutokana na askari wa Jiji kuendesha operesheni husika kwa fujo na uporaji.

Eneo la Mwanjelwa limekuwa ngome kuu ya Chadema tangu mwaka 2011, zilipoibuka vurugu za kwanza kubwa kufanywa na machinga na kusababisha shughuli zote ndani ya jiji hilo kusimama kwa takribani juma moja, ikiwemo kusimama kwa shughuli zote za usafirishaji, kutoka na kuingia mkoani Mbeya pamoja na safari za nchi jirani.

Katika vurugu hizo, zinazoelezwa kuchangiwa zaidi na hasira ya baadhi ya vigogo wa CCM zilizotokana na kupoteza jimbo hilo kwa Chadema, nguvu kubwa ya dola ilitumika kudhibiti bila mafanikio, na kulazimika kumtumia Mbunge wa Jimbo hilo, Joseph Mbilinyi kutuliza.

Tukio hilo ndilo linaelezwa kumnyanyua mbunge huyo na kuhitimisha umaarufu wa CCM katika siasa za Jiji la Mbeya. Ndizo vurugu zilizosababisha aitwe ‘Rais’ wa Mbeya, na madhara yake kwa CCM yameendela kukitafuna hadi leo.

Tangu wakati huo, serikali mkoani Mbeya imekuwa haina nguvu mbele ya wafanyabiashara hao, ambapo ilifikia hatua ya kila wanachokiamua waliachiwa waendelee, ikiwemo kuweka bidhaa zao popote walipopenda wao, hata kama itakuwa ni kuzuia barabara, walipanga kwenye miti hadi maduka ya wafanyabiashara wengine.

Kwao biashara ilikuwa popote na walipozuiwa walitishia kufanya vurugu. Kipindi chote hicho walifurahia nguvu yao, na Chadema walifurahia wakiuona kuwa mtaji wao wa kisiasa wakati CCM walihofia kuendelea kuporomoka, hivyo nao wakaibana serikali yake kutowaudhi machinga.
Chadema walifanikiwa, walipata mtaji na uthibitisho ni Uchaguzi Mkuu uliopita ambapo CCM wamelazimika kukaa upande wa kambi ya upinzani ndani ya Baraza la Madiwani la Jiji hilo.

Fungate limeisha, sasa Chadema wanawajibika kusimamia sheria, mtaji wao taratibu unageuka kuwa shubiri.

Baadhi ya machinga hao wameanza kulalamika, kwamba chama chao walichokichagua kutokana na ahadi ya kuendelea kuwasimamia, nacho kimewageuka na kuanza kuwashughulikia.

Kigogo mmoja wa chama hicho anauangalia mgogoro huo kwa jicho la hadhari, anauona kuwa tishio kwa chama chao, akisema wanatakiwa kuwatumikia wananchi wao, lakini lazima wasimamie sheria na kutoa ushirikiano kwa watendaji, vinginevyo chama chao ndicho kitaathirika.

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Chadema kilizoa kata nyingi zaidi pamoja na jimbo, ndio wenye kuongoza Baraza la Madiwani, sasa wanajikuta njia panda, wasimamie sheria au waendeleze falsafa yao ya “People’s power,” jiji lisitawalike.

Vyanzo vya ndani vya chama hicho vinabainisha kuwa baadhi ya madiwani wa Chadema, Baraza lililopita, walianza kuliona tatizo hilo, hivyo kupinga harakati zozote za kutetea vurugu za machinga zenye kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara na mali za Jiji na watu wake.

Rai Mwema
 
nilichokiona toka mwanzo hadi mwisho wa utunzi huu ni....uchonganishi tu
 
Kama wananchi wanaharibu miundo mbinu, waachwe waisome namba, simpo! Kwanza sijasikia MASTER PLAN ya jiji la mbeya kutoka kwa Likuvi juzi juzi.
 
Back
Top Bottom