Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,717
- 4,458
Wakuu,
Baada ya Shinyanga kutangaza kuwa wanamuunga mkono Tundu Lissu naona na Mwanza nao wameunga mkono juhudi
==========================================================
Wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Mwanza wamemuomba Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe kutokugombea tena nafasi hiyo na badala yake kuwapisha wanachama wengine.
Wajumbe hao wakizungumza mbele ya wanahabari wametangaza wazi kumuunga mkono Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Lissu aliyetangaza nia ya kugombea uenyekiti taifa hivi karibuni, na kueleza kuwa Mbowe anapaswa kupumzika kwa heshima baada ya kukiongoza chama kwa muda mrefu.
Aidha, wamemkana Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo aliyeungana na viongozi wengine kwenda
kumshinikiza Freeman Mbowe kugombea wakidai kuwa wao hawakumtuma na wala hawamuungi mkono.